Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania
(FONATA) Prof. Joyce Kinabo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam, kuhusu Mkutano wa tatu wa Shirikisho
la Vyama vya Wataalamu wa Masuala ya
Chakula na Lishe Afrika ambao unalenga kutoa fursa kwa wanasansi wa masuala ya
lishe ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Chakula na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda na
Afisa Mawasiliano wa taasisi hiyo Herbert Gowelle (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula
na Lishe Dkt. Joyceline Kaganda akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu namna
taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia umuhimu wa lishe
nchini kama moja ya masuala muhimu ya
kimaendeleo. Kushoto ni Rais wa Chama
cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo.
Rais
wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu kupunguza
viwango vya ukondefu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa
asilimia 50 mwishoni mwa mwaka huu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo Dkt. Joyceline Kaganda.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa taasisi ya chakula na lishe
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment