TANGAZO


Thursday, May 21, 2015

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu atoa madawati 270 kwa Sekondari za Jimbo lake

Baadhi ya madawati 270 yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa ajili ya Shule za Sekondari, zilizopo kwenye Jimbo lake hilo. Madawati hayo, aliyanunua kwa Sh. mil. 60.  
Mbunge wa Jimbo la  Temeke, Abbas Mtemvu (mwenye kapero), akikabidhiwa madawati na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta), Samuel Ng'andu, Dar es Salaam juzi, baada ya mbunge huyo, amenunua madawati 270 kwa ajili ya shule za Sekondari, zilizopo jimboni mwake.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kuyanunua Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) na kuyakabidhi kwa Madiwani  wa Jimbo hilo.
Diwani wa Kata ya Keko, Frances Mtawa (kushoto), akimshukuru Mkuu wa chuo hicho, kutokana na kulishughulikia tatizo hilo la madawati kuyafanyia kazi kupatikana kwa muda muafaka. Pia alimshukuru Mbunge wake, Abbas Mtemvu kwakuwa muwazi na kuwashirikisha madiwani wa jimbo hilo, katika suala hilo. Kulia ni Mkuu wa chuo cha Ufundi Stadi (Veta) na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu. (Picha zote na Khamisi Mussa)

No comments:

Post a Comment