Baadhi ya wasanii wa vikundi vya sanaa na wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya uanuai wa Utamaduni Dunia.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko Mkurugenzi kizungumza wakiti wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline Maleko na mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw.
Wapiga vyombo vya muziki na ngoma kutoka kikundi cha Tanzania wakichakarika wakati wa zoezi la kutumbia kwenye hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya uanuai wa Utamaduni.
Wanakikundi cha sanaa kutoka nchini India wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniaa ambayo nufanyika kila tarehe 21 mwezi wa tano kila mwaka.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermsa Mwansoko akicheza Bao na Balozi wa India nchini Bw. Debnath Shaw wakati wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameambatana na maonyesho ya wajisariamali wa bidhaa za kiutamaduni na kuratibiwa kwa ushirikianao baiona ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni na Tan Trade.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akiangalia namna wanafunzi wa Shule ya Msingi Magomeni wanavyochora michoro mbalimbalai wakati wa maonyesho ya ujasiriamali wa kiutamaduni ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha zote na Frank Shija, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)
WADAU mbalimbali wa sekta ya Utamaduni nchini wameiomba jamii kuuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa kuzingatia matumizi ya vitu vinavyoendana na tamaduni za Tanzania ili kudumisha na kuenzi mila na desturi za Tanzania.
Kauli hiyo imeibuliwa na wadau wa sekta ya Utamaduni walioshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 21 ya mwezi Mei ambapo Tanzania imeadhimisha siku hiyo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi. Jacqueline Maleko ameiomba serikali kujenga kituo cha Utamaduni kitakachotumika kuendeleza, kudumisha na kuhamasisha matumizi ya vitu vya asili ya Tanzania hivyo kuendeleza tamaduni zetu.
“Utamaduni wa mtanzania ni urithi wenye mashiko kama utadumishwa na kuhamasisha jamii kutumia vitu vya asili kama vile nyimbo, ngoma, uchongaji, mashahiri, uchoraji, filamu Sanaa,
vyakula na mavazi kwa kuviendeleza na kuvinadi ndani na nje ya Tanzania” Amesema Bibi Maleko.
Akitoa maoni yake kuhusu utamaduni wa Tanzania Mwalimu Gasper Maro kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa shule za msingi zimekuwa zikijitahidi kuuenzi utamaduni wa Tanzania kwa kuwahamasisha wanafunzi kuimba nyimbo za jadi na kucheza ngoma za makabila mbalimbali ili kuweza kujua tamaduni za kila kabila lililopo nchini Tanzania,
Hata hivyo mwalimu Maro amesema kuwa utamaduni wa Tanzania kwa sasa unashuka kutokana na kizazi cha sasa kuiga tamaduni za nchi nyingine na kudharau tamaduni zao hivyo kuwaomba maafisa utamaduni nchini kuandaa programu mbalimbali zitakazokuwa zikihamasisha jamii kuishi kwa kufuata tamaduni za Tanzania.
Kwa upande wake mwanafunzi Agustino George Pius kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa utamaduni wa Tanzania umekua ukibadilishwa na vijana kutokana na maendeleo ya teknolojia hasa katika upande wa mavazi, vyakula, pamoja na staili ya maisha wanayoishi vijana wa sasa.
Naye Afisa Utumishi kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTO) Bw. Elius Ngemela ameitaka jamii kutambua kuwa utamaduni ni utambulisho wa nchi ambao kama utatumika vizuri utasaidia kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira katika jamii hivyo kuuthamini na kuudumisha kwa maendeleo ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment