TANGAZO

Tuesday, May 5, 2015

DC Makonda aumaliza mgomo wa madereva wa mabasi ya kwenda mikoani jijini Dar es Salaam

Askari wa kutuliza ghasia wakiwa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani, Ubungo, Dar es Salaam jana katika kuimarisha ulinzi wakati wa mgomo wa madereva wa mabasi hayo jijini leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Askari wa kutuliza ghasia wakiwa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani, Ubungo, Dar es Salaam leo, tayari kwa ajili ya kuyasindikiza mabasi ya kwenda Dodoma ya Kampuni ya Shabiby wakati yalipoanza safari zake ya kwenda mkoani humo leo kabla ya mgomo wa madereva kutatuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuutatua mgogoro huo kituoni hapo leo.
 Basi la Shabiby likiondoka kituo cha Ubungo tayari kwa safari ya kwenda mkoani Dodoma leo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza jambo, akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (wa pili kushoto) na viongozi wa madereva, wakati alipokuwa akitafuta maelewano na uongozi huo kuhusu kusitisha mgomo wao wa kutotoa huduma za usafirishaji abiria, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa madereva, Clement Masanja. 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akienda kwenye mkutano wa madereva wa daladala DC Makonda wakati alipokwenda kuwaeleza makubaliano yao na viongozi wao. 
Katibu wa Madereva akiwasalimia na kuzungumza na madereva wa mabasi ya mikoani 

Madereva wa mabasi ya kwenda mikoani, waliokuwa wamegoma, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wakati alipokuwa akizungumza nao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akizungumza na madereva wa mabasi ya kwenda mikoani kuwaeleza makubaliano yao na viongozi wao kuhusu makubaliano yao ya kusitisha mgomo na kuendelea kutoa huduma ya usafirishaji abiria.
Madereva wa mabasi ya kwenda mikoani, waliokuwa wamegoma, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wakati alipokuwa akizungumza nao. 

Mabasi ya mikoani yakiondoka kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo mara baada ya uongozi wake kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuhusu kusitisha mgomo wao na kuendelea na kutoa huduma ya usafiri kwa wasafiri wa mikoani jijini leo.
Wananchi wakishangilia wakati basi la Kampuni ya OTA Classic, likitoka Kituo cha Mabasi ya kwenda mikoani, Dar es Salaam leo, kuanza safari zake za kuelekea Bukoba baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuzungumza na viongozi wa madereva waliokuwa wamegoma na kukubaliana kusitisha mgomo wao na kuendelea kutoa huduma ya usafirishaji abiria. 

Mabasi ya mikoani yakiondoka kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo mara baada ya uongozi wake kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuhusu kusitisha mgomo wao na kuendelea na kutoa huduma ya usafiri kwa wasafiri wa mikoani jijini leo. 
 Mabasi ya mikoani yakiondoka kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo mara baada ya uongozi wake kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuhusu kusitisha mgomo wao na kuendelea na kutoa huduma ya usafiri kwa wasafiri wa mikoani jijini leo.

 Mabasi ya mikoani yakiondoka kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo mara baada ya uongozi wake kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuhusu kusitisha mgomo wao na kuendelea na kutoa huduma ya usafiri kwa wasafiri wa mikoani jijini leo.

Kijana akiwa ameshikiliwa na askari kanzu kituoni hapo, baada ya kuhisiwa kutaka kufanya vurugu wakati mabasi ya kwenda Dodoma ya Kampuni ya Al Shabiby yakianza safari zake leo. 

Mabasi ya mikoani yakiondoka kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo mara baada ya uongozi wake kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuhusu kusitisha mgomo wao na kuendelea na kutoa huduma ya usafiri kwa wasafiri wa mikoani jijini leo.

No comments:

Post a Comment