TANGAZO


Thursday, May 21, 2015

Australia haitawaruhusu Rohingya kuishi

Australia haitawaruhusu Rohingya kuishi nchini humo
Australia imeonya kuwa haitawaruhusu wakimbizi wa jamii ya waislamu wa Rohingya waliowasili nchini humo kwa mashua kuishi.
Waziri mkuu, wa nchi hiyo Tony Abbott, anasema kuwa ni muhimu mataifa ya magharibi kutafuta mbinu ya kuzuia ulanguzi wa watu.
Anasema, njia pekee ni kuhakikisha kuwa hakuna mashua ambayo inawabeba wahamiaji hadi katika taifa lolote la magharibi.
Bwana Abbott anasema watu wanaotafuta uhamiaji wanafaa kufuata njia rasmi kuhusu uhamiaji.
Abbott :Hatutakubali wahamiaji hao wa Rohingya kuishi nchini mwetu
''Haiwezekani eti kwa sababu umepanda mashua hafifu naambayo inavuja maji utatua nchi yeyote ya magharibi na unaanza maisha mapya !
haiwezekani'' alisema bwana Abbott.
''Ni wajibu wetu kila mmoja kuhakikisha kuwa tunakabiliana na ulanguzi wa watu'' aliongezea.
Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Malaysia na Indonesia wamo nchini Myanmar kwa ajili ya mazungumzo kuhusu tatizo hilo la wahamiaji.
Takriban watu 7,000 wanaaminika kuwa wamekwama baharini.
Takriban watu 7,000 wanaaminika kuwa wamekwama baharini.
Wahamiaji hao wanajumuisha waislamu wa kabila la Rohingya wanaotoroka mateso pamoja na kuhangaishwa nchini Myanmar.
Wapo pia raia wa Bangladesh, ambao wanadhaniwa kuwa wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya kiuchumi.
Malaysia pamoja na Indonesia zimesema kuwa zitatoa hifadhi ya muda kwa wale watakao wasili katika maeneo yao, lakini zinahitaji msaada kutoka jamii ya kimataifa kuwasaidia kuwapa makaazi.

No comments:

Post a Comment