TANGAZO


Monday, March 16, 2015

Waziri Fenella azindua Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) na wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno iliyofanyika katika viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya hiari yaliyoanzia katika viwanja hivyo na kupitia Barabara ya Diomond Jubilee kabla ya kurudi uwanjani hapo kupitia barabara ya Alhasan Mwinyi na Kauli mbiu ya wiki ya Afya ya Kinywa ni “Tabasamu la Maisha” Katikati ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro na wa mwisho kulia ni Rais Mteule wa Chama hicho Dkt. Ambege Mwakatobe. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akipeana mkono na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro (kulia) jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. 
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiangalia baadhi ya machapisho yanayohusu Afya ya Kinywa na Meno kwenye banda lililowekwa katika Viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kushoto ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wapili kutoka kushoto) akiwa katika matembezi ya amani ikiwa ni katika hfla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) katikati akiingia katika viwanja vya Salender Bridge Club wmara baada ya kumalizika kwa matembezi ya amani yaliyolenga kuhamasisha umma kuhusu kujali afya zao jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kulia ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carnei
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wkishiriki matembezi ya amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wapili kutoka kulia) akiwa katika matembezi ya amani ikiwa ni katika hfla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment