TANGAZO


Monday, March 16, 2015

Viongozi wa Albino Manispaa ya Iringa wambariki Frank Kibiki katika harakati zake za kugombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini

 Mwanahabari Frank Kibiki, aliyewahi kuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ngazi ya Wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa NEC.

Na Mwandishi wetu, Iringa

WANANCHI wa manispaa ya iringa wamempongeza , Frank Kibiki kwa kuanzisha mashindano ambayo yalengo la kuwataka wakazi wa mkoa wa iringa kujua kuwa albino ni binadamu kama binadamu wengine hivyo tunatakiwa kuacha kuwauwa na kuwa nyanyasa kijinsia.
Wakizungu kwa nyakati tofauti na blog hii wamesema kuwa wazo la mbunge mtarajiwa la kutoa elimu ya kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)  kwa njia ya michezo yatawasaidia wakazi wa manispaa kwa kuwa wananchi wengi wanapenda michezo hivyo itakuwa rahisi kuwafikia.

Pia walimtaka FRANK KIBIKI kuendelea na harakati za kupigania na kuwania ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anakila sababu ya kufanya hivyo kutokana na malengo pamoja na msimamo anaouonyesha kwa wakazi wa manispaa.

 Kwa upande wao viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)  mkoani iringa wamempongeza na kumuomba katika mashindano hayo wanaomba timu yao ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)kuwa moja kati ya timu itakayoshiriki katika mashindano hayo.
“Tunaomba nasi kushiriki katika mashindano hayo ya Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 kwa kuwa ujumbe wa mashindano hayo unatulenga sisi, hivyo haitakuwa busara mashindano yaendelee bila sisi kuleta timu uwanjani”walisema viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) waliwataka wananchi wa manispaa ya iringa kumuunga mkono frank kibiki katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anaoneka kabisa kuwajari wananchi wenye kipato kidogo tofauti na wale wagombea wengine ambao wanatumia pesa nyingi kuutaka ubunge wa jimbo hilo.

Walimalizia kwa kusema kuwa kesho watapeleka barua maalum kwa frank kibiki ya kumpongeza na kuwaomba wananchi wengine kumuunga mkono kibiki ili kuyafanya mashindano hayo kuwa bora zaidi.
Naye Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.

Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.

lakini kibiki hakusita kuwashukuru viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)mkoani iringa kwa kutambua lengo lake japo bado ajaletewa rasmi barua hiyo ya pongezi kwa naye amesikia tu kwa wananchi wakimshukuru kwa elimu na ujumbe aliouweka katika mashindano yake.



Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.

No comments:

Post a Comment