TANGAZO


Tuesday, March 3, 2015

US:Sudan Kusini sharti ihakiki Makubaliano

Marekani yaonya kuwa itachukua hatua kali dhidi ya pande zote
Marekani imeonya kuwa itachukua hatua dhidi ya pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini iwapo hazitaafikia makubaliano ya amani kufikia alhamisi wiki hii.
Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry ameonya kuwa mapigano ni lazima yamalizike mara moja.
Ameyasema hayo huku Rais Salva Kiir akiwasili jijini Addis Ababa kwa mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi wa Waasi Dkt Riek Machar, baada ya kukosa kuhudhuria kikao cha ufunguzi wa awamu hii ya mwisho ya mazungumzo.
Katika taarifa Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry amewakashifu rais Kiir na kiongozi wa Waasi Machar kwa kushindwa kuafikia mkataba wa amani.
Amewataka wawili hao kuweka masilahi ya raia wa Sudan Kusini mbele na kutia saini makubaliano ya amani ya kudumu.
Kerry amesema kuwa wahusika wote sharti watekeleza makubaliano.
Kerry ameonya kuwa Marekani itashirikiana na mataifa ya kanda hili na Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote anayehujumu kupatikana kwa mani Sudan Kusini. Lakini hii si mara ya kwanza kwa Marekani kutoa vitisho kama hivyo.
Tayari Marekani na Muungano wa Ulaya EU imewawekea vikwazo makamanda kadhaa kutoka pande zote mbili na pia imewasilisha pendekezo ya adhabu zaidi dhidi ya viongozi hao katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Rais Kiir na Dkt Machar wanakutana hii leo kwa awamu ya mwisho ya mazungumzo ya kubuni serikali ya mpito na kumaliza takriban miezi kumi na mine ya mapigano nchini humo.
Maelfu ya watu wameuwawa na wengine zaidi ya milioni moja unusu kufurushwa makwao tangu mapigano kuzuka nchini humo Desemba mwaka wa 2013.

No comments:

Post a Comment