TANGAZO


Sunday, March 15, 2015

Ubalozi wa US, Saudia wasitisha huduma


Ubalozi wa marekani nchini saudi Arabia umesitisha huduma zake kwa sababu za kiusalama

Ubalozi wa Marekani kwenye mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh umesitisha huduma zake zote kwa leo jumapili na kesho jumatatu kutokana na sababu za kiusalama.
Kupitia taarifa kwenye mtandao wake, ubalozi huo umesema kuwa huduma kwenye ofisi zake katika miji ya Riyadh, Jeddah na Dhahran hazitakuwepo.
Umewashauri raia wote wa Marekani kuchukua tahadhari zaidi wakisafiri kote nchini Saudi Arabia.
Mapema jana Jumamosi ubalozi huo ulionya kuwa wafanyikazi wa sekta ya mafuta kutoka nchi za magharibi wanaweza kulengwa na magaidi kwenye mkoa wa mashariki wenye utajiri wa mafuta.

No comments:

Post a Comment