Mratibu wa Tamasha la Karibu International Music Festival, Richard Lupia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha la pili litakalofanyika mwezi Novemba mwaka huu katika viwanja vya Mwanakalenge Bagamoyo. Tamasha hilo limeandaliwa na Taasisi ya Karibu Cultural Promotion na kuratibiwa na Kampuni ya Legendary Music Entertainment. Kulia ni Ofisa Habari wa Kampuni ya Karibu International Music Festival, Said Hashim.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
TAMASHA la Music Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 6 hadi 8 mwaka huu, Bagamoyo mkoani Pwani katika viwanja vya Mwanakalenge.
Akizungumza Dar es Salaam leo Meneja wa Tamasha hilo Richard Lupia alisema lengo ni kukazia katika kurasimisha tasnia ya muziki kuwa na umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo husika la bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
Pia Lupia alisema kuunganisha wanamuziki na kufanya sanaa ya asili ya Tanzania inapata kuonekana katika jukwaa la kimataifa.
Lupia aliendelea kusema Tamasha litashirikisha vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 ndani na nje yanchi wanaopiga muziki wa dansi, Reggae, Hip Hop, Taarab,Ngoma za Asili, Bongofleva na Ghani.
"Wasanii watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbalimbali ambapo kutakua na warsa kutoka kwa wataalamu mbalimbali kutoka pande zote za dunia" alisema.
Aidha tamasha litaendeshwa mchana na usiku ambapo mchana kutakuwa na sanaa za michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha huku semina na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine za kimaendeleo zikiendelea.
"Tushirikiane katika kuhakikisha muziki wa Tanzania unafika katika kilele cha mafanikio pia nafasi za maombi ya ushiriki kwa wasanii bado zipo" alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment