TANGAZO


Saturday, March 14, 2015

Simba yaipiga Mtibwa kama Yanga Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

*Okwi apiga bao la mbali kama alivyoifunga Yanga
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Mtibwa Sugar ya Morogoro, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Simba imeshinda bao 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji wake hatari, Emmanuel Okwi kutoka Uganda. Okwi amefunga bao hilo kwa staili ile ile aliyoifunga Yanga watani wa jadi wa Simba, bao la mbali, mpira aliouweka pembeni mwa goli baada ya kumchulia golikipa sehemu aliyokaa na kisha kuupiga mpira kwenye kona ya juu ya goli kushoto kwa golikipa, ikiwa ni dakika ya 89 ya mchezo huo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Mtibwa Sugar ya Morogoro, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.  
Emmanuel Okwi akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar. 
Emmanuel Okwi akimtoka Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.  
Emmanuel Okwi akiupiga krosi mpira huku akiwa bado anakifuatwa na Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.  
Kessy Ramadhan wa Simba akiudhibiti mpira huku akizongwa na kapteni wa Mtibwa Sugar.
Kessy Ramadhan wa Simba akimtoka kapteni wa Mtibwa Sugar.
Kapteni wa Mtibwa Sugar akiuondoa mpira miguuni mwa Kessy Ramadhan wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu hiyo na Mtibwa Sugar ya Morogoro, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Elius Maguri wa Simba akimpiga chenga Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.
Elius Maguri wa Simba akimtoka Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.
Elius Maguri wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.
Elius Maguri wa Simba akijaribu kumpiga chenga Andrew Chikupe wa Mtibwa Sugar.
Mussa Hassan Mgosi wa Mtibwa Sugar akiwania kuutoa mpira miguuni mwa Awadh Juma wa Simba.
Emmanuel Okwi akiwa amedondoshwa chini huku Ramadhan Singano wa Simba akiudhibiti mpira akiwa amezongwa na wachezaji wa Mtibwa Sugar.
Henri Joseph wa Mtibwa Sugar, akijaribu kumdhibiti Emmanuel Okwi wa Simba.
Henri Joseph wa Mtibwa Sugar na Emmanuel Okwi wa Simba wakiwania mpira.
Emmanuel Okwi wa Simba akijaribu mbinu ya kumtoka David Luhende wa Mtibwa Sugar.
Emmanuel Okwi wa Simba akiwa na mpira akimfuata David Luhende wa Mtibwa Sugar.
Golikipa wa Mtibw Saidi Saidi akipatiwa matibabu baada ya kugongana na mchezaji wa Simba, Emmanuel Okwi (kulia), wakati akijaribu kuudaka mpira wa juu.
Emmanuel Okwi wa Simba akiwania mpira na David Luhende wa Mtibwa Sugar.
Golikipa wa Saidi Saidi wa Mtibwa akiwa amechanganyikiwa baada ya kufungwa kwa mpira wa mbali na Emmanuel Okwi, ikiwa na bao pekee katika mchezo huo, katika dakika ya 89 ya mchezo huo na hivyo Simba kujipatia pointi 3 muhimu katika mchezo huo.
Mchezaji wa Simba, Said Ndemla akishangilia bao lililofungwa na Emmanuel Okwi wa timu hiyo katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao hilo pekee katika mchezo huo, lililoipatia timu yao pointi 3 muhimu.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao hilo pekee katika mchezo huo, lililoipatia timu yao pointi 3 muhimu.

Ramadhan Singano na Emmanuel Okwi wakishangilia bao hilo kwa staili yake.
Ramadhan Singano akimpongeza mfungaji wa bao hilo, Emmanuel Okwi wakati wakishangilia kwa staili ya kipekee.
Ubao wa matangazo ukuinesha Simba bao 1 na Mtibwa Sugar 0 hadi mwisho wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakifurahia bao lililofungwa na Emmael Okwi katika mchezo huo kati ya timu hiyo na Mtibwa Sugar ya Morogoro, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.

No comments:

Post a Comment