Mwili wa mwandishi wa habari, Fatuma Gaffus ukipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda kuzikwa katika Makaburi ya Makubeli, Kikuyu, Dodoma jana.
Waombolezaji wakilipakia jeneza lenye mwili wa marehemu Fatuma Gaffus kwenye gari tayari kwa ajili ya kwenda kuuzika katika Makaburi ya Makubeli, Kikuyu, Dodoma jana.
Na John Banda, Dodoma
SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu jana aliwaongoza Mamia ya Waombolezaji kumzika mwandishi na mtangazaji mkongwe nchini Fatuma Gaffus katika mazishi yaliyofanyika katika Makaburi ya Makuberi, Kikuyu, mkoani Dodoma.
Gaffus ambaye alifariki juzi katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa kwa muda akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo pamoja na upungufu wa Damu.
Akizungumza wakati wa sala ya kumswalia marehemu iliyofanyika katika Msikiti wa Majengo Shekhe huyo wa Mkoa aliiwata waandishi kuendelea na kazi kama aliyofanya marehemu ya kuupigania uislamu kwa hali na mali.
Alisema jamii inatakiwa iwe na subira katika kila jambo kwani kila jambo anapanga mwenyezi mungu hivyo kile anachofanya ana makusudio yake na anatakiwa kushukuliwa.
‘’Marehemu nilimjua tangu siku nyingi alikuwa akiupigania uislamu kwa hali na mali mpaka hata marehemu mama yake naye aliupigania uislamu tunakiwa tuige mfano kama wake na sisi siku mungu akituchua jamii itukubali kama tunavyofanya leo kwa Fatuma’’
‘’Tunatakiwa kutenda matendo mema ya kumpendeza mungu,pia tunatakiwa tuwe na subira,umeondokewa na Mama,Baba,Mwana subira ndio jambo la msingi,ila niwaambie na nyie mliopo hapa mmejiandaaje na mauti kwani kila nafsi itaonja mauti’’alisema Shekhe huyo wa Mkoa.
Kwa upande wake Mwandishi Mkongwe ambaye aliyemfundisha Marehemu kazi ya Utangazaji na uandishi Daniel Msangya alisema alimfahamu kwa muda mrefu marehemu na kudai alikuwa ni mtu aliyejituma na alifahamu misingi ya kazi zake.
Alisema fani ya Uandishi imepata pengo kubwa kutokana na kuondokewa na mpambanaji ambaye katu pengo lake haliwezi kuzibika kutokana na jinsi alivyokuwa akijituma.
‘’Nimepokea msiba huu kwa majonzi kwani mimi ndio mwalimu wake wa kwanza wa uandishi na utangazaji na yeye akawa mpambanaji jina lake lilikuwa halikosekani katika vipindi vya Radia Free na Star tv tangu ametoka kule vipindi vimepwaya sana kutokea Dodoma’’
‘’Alikuwa anapenda kujiendeleza kielimu mpaka akafikia ngazi ya Diploma, pia alikuwa Mbobezi maana alibobea katika uandishi wa michezo kitu kilichomtanulia wigo mkubwa wa vyanzo vya habari na hata ukikutana nae wakati wote yupo kazini, ila tumempoteza Jembe [mtu muhimu] katika tasnia ya Habari’’alisema Msangya.
No comments:
Post a Comment