TANGAZO


Thursday, March 12, 2015

Rais Kikwete awaapisha Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi, kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, wakati alipokuwa akiwaapisha makamishna wa tume hiyo, Ikulu, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Makamishna wapya wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete ili awaapishe kuwa akamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Wageni mbalimbali waalikwa, wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wageni, ndugu na marafiki wa Kamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, wakisubiri ndugu zao kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Utumishi wa Umma, Steven Bwana, wakati alipowaapisha Makamishna wapya wa tume hiyo, Ikulu Dar es Salaam leo
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mgeni Mwalimu Ali, wakati alipokuwa akiwaapisha makamishna wa tume hiyo, Ikulu, Dar es Salaam leo. 
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Alhaj Yahya Mbila, wakati alipokuwa akiwaapisha makamishna wa tume hiyo, Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha Evelyne Ianisa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, wakati alipokuwa akiwaapisha makamishna wa tume hiyo, Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi vitendea kazi Adieu Nyondo mara baada ya kumwapisha kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha Salome Mollel kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi vitendea kazi Salome Mollel mara baada ya kumwapisha kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ikulu, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (watano kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (wanne kulia), mara baada ya kuwaapisha makamishna hao, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na makamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Umma, mara baada ya kuwaapisha, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma (wenye maua), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa na watumishi wa ofisi hiyo, mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment