Rais anayeondoka madarakani nchini Namibia Hifikepunye Pohamba, 79,ameshinda tuzo ya dola milioni tano ya Mo Ibrahimu ya uongozi wa Afrika.
Tuzo hiyo ya dola milioni 5 hutuzwa kiongozi wa Kiafrika aliyechaguliwa na anayeongoza kwa njia bora na kuinua maisha ya watu na kuondoka ofisini
Bwana Pohamba ambaye anaondoka madarakani baadaye mwezi huu ndiye mwanzilishi wa kundi la SWAPO lililopigania uhuru wa Namibia.
Rais huyo anatarajiwa kumkabidhi madaraka rais mteule Hage Geingob.
Pohamba amehudumu vipindi wili kama rais wa Namibia alipo chaguliwa kwanza mwaka wa 2004 na tena mwaka wa 2009.
Mwanabiashara raia wa Sudan Mo Ibrahim ndiye alizindua tuzo hilo kuwapa motisha viongozi wa Afrika kuondoka madarakani kwa njia ya amani.
Aliyekuwa rais wa Msumbiji Joaquim Chissano ndiye aliyetuzwa kwanza mwaka wa 2007na ndiye alichangia pakubwa kwa kujaribu kutafuta uwiano baina ya viongozi kadhaa barani Afrika
Mmoja wa wanajopo wanaoteua marais wanaopewa tuzo hilo Salim Ahmed Salim amemtaja Pohamba kama mtu aliyeiunua maisha ya watu wake
Mshindi anapokea dola milioni 5 ambayo huwa inagawanywa ilikutolewa katika kipindi cha muongo mmoja kisha washindi wanatuzwa dola lakimi mbili kila mwaka hadi siku ya kufa.
No comments:
Post a Comment