TANGAZO


Sunday, March 1, 2015

Mkataba wa amani Mali wakubaliwa nusu

Wanajeshi wa Mali
Ushirika muhimu wa makundi ya watu wa kabila la Tuareg wa Mali, umekataa kutia saini mswada wa mkataba wa amani uliolenga kuleta utulivu kaskazini mwa nchi.
Makundi hayo ya Watuareg yameomba kupewa muda zaidi kuwashauari wafuasi wao.
Makundi mengine sita yaliyokuwa yakitaka kujitenga yametia saini makubaliano hayo, ambayo yanaruhusu madaraka fulani ya serikali yagawiwe kwa eneo la kaskazini; lakini hautoi uhuru kamili kwa eneo la kaskazini.
Wanajeshi wa Ufaransa na nchi za Afrika waliingilia kati nchini Mali Januari 2013 ili kuzuwia wapiganaji waliokuwa na uhusiano na al-Qaeda wasisonge kusini hadi mji mkuu, Bamako - lakini makundi ya wapiganaji wa kabila la Tuareg na ya Waislamu yamekuwa yakiendelea na harakati zao
Mkataba wa sasa unafuatia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutishia kuziwekea vikwazo pande zote zinazohusika.

No comments:

Post a Comment