TANGAZO


Thursday, March 12, 2015

Jeshi la Iraq lapiga hatua dhidi ya IS

Wanajeshi wa Iraq wamepiga hatua kubwa katika harakati za kuuteka mji wa Tikrit unaodhibitiwa na wa IS
Taarifa za kiusalama zinaarifu kuwa majeshi ya nchi ya Iraq kwa mara nyingine tena, yamepiga hatua kubwa katika juhudi zao za kuutwa kabisa mji wa Tikrit kutoka kwa wanamgambo wa Islamic State.
Jeshi linasema, vikosi vyake viliingia kwa miguu, magari na vifaru kote pembezoni mwa mji huo, kuelekea katikati mwa Tikrit.
Mji huo ni nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Iraq, hayati Saddam Hussein.
Mapigano yanaendelea katika viunga vya mji huo yakiwemo Ikulu ya zamani ya Saddam Hussein.
Tikrit ndio ngome kuu la IS, huku waandishi habari wakisema kuwa, iwapo serikali ya Iraq itafauluu kuchukua umiliki wa mji huo, itakuwa hatua kubwa mno.

No comments:

Post a Comment