Misri imetekeleza hukumu ya kifo ya mwanzo, iliyotolewa baada ya kupinduliwa kwa serikali ya rais muislamu, Mohammed Morsi, miaka miwili iliyopita.
Muislamu mwenye siasa kali, Mahmoud Hassan Ramadan, alinyongwa, baada ya kuhukumiwa kwa kuhusika na mauaji.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri, imesema kuwa mashtaka yalihusika na tukio, ambapo watu wawili walirushwa kutoka katika jengo, wakati wa ghasia za kupinga Morsi kuondolewa madarakani.
Mahakama ya Misri imetoa hukumu ya kifo kwa mamia ya wale wanaosemekana ni wafuasi wa Muslim Brotherhood, baada ya kesi za haraka, ambazo mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu na serikali za nchi za nje, zinasema hazikuwa sawa.
No comments:
Post a Comment