Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasalimia wadau wa Utamaduni huku akiwa ameshika moja ya dhana za utamaduni alipokua akifungua kikao cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wadau wa Utamaduni alipokua akifungua kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
Baadhi ya wadau wa Utamaduni kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea katika kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni jana jijini Dar es Salaam.
Ofisa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya Bw. Godfrey Msokwa akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Lugha Bibi Shani Kitogo.
Mmoja wa washairi (kushoto) akiburudisha wadau wa Utamaduni wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma kijulikanacho kama Jivunie Sanaa Tanzania kikitumbuiza wakati wa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa
mwenye suti) katika picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Utamaduni baada ya
kufungua kikao kazi cha kumi cha Sekta hiyo jana jijini Dar es Salaam. (Picha
zote na Genofeva Matemu – Maelezo)
Na Genofeva Matemu – Maelezo
Tarehe 05/03/2015
MAOFISA Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kutumia sanaa kupitia fani
mbalimbali kuhamasisha juhudi za kuifahamu na kuipokea katiba inayopendekezwa
ili jamii ya watanzania kuweza kujipatia katiba inayokidhi mahitaji yao.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua kikao kazi cha kumi cha Sekta
ya Utamaduni, Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Profesa
Gabriel amesema kuwa lengo la kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni ni kutanabaisha
maudhui ya Katiba inayopendekezwa hivyo kuwataka wadau wa utamaduni kutumia
tasnia ya sanaa inayoumbwa na herufi K
tatu zinazolenga Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha jamii katika masuala mbalimbali.
“Utamaduni
ni kama inta inayoshikamanisha watu, ni vyema wadau wa utamaduni mkatumia
talanta mliyonayo kufikia fikra za watu kwani suala la katiba pendekezwa ni
letu sote kama watanzania hivyo tujivunie kwa kuweka mambo kwenye vitendo na
kuishi yale tunayoyasema” amesema Profesa Gabriel.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni
Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa sanaa imekua ikitumika kusaidia makundi
mbalimbali katika jamii kutoa sauti zao kwenye mambo mbalimbali na kuamini kuwa
sanaa ina nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii maudhui ya katiba
inayopendekezwa.
Bibi.
Kihindu amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kimewashirikisha maafisa
utamaduni kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kikiwa na madhumuni ya kueleza
mchango wa fani za sanaa katika kuelimisha umma maudhui ya katiba
inayopendekezwa na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Utamaduni
yaliyozingatiwa katika Katiba inayopendekezwa.
Akizungumza
kwa niaba ya maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara, Afisa
Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa amesema kuwa
kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kitawawezesha wadau wa utamaduni kutumia
sanaa kuifikia jamii na kutekeleza maazimio yatakayokusudiwa na kikao hicho.
Kikao
kazi cha 10 cha Sekta ya Utamaduni chenye kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa
zielimishe Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa kimelenga kutumia sanaa kama
kichocheo na mbinu mojawapo ya kuelimisha, kuonya na kuelekeza mambo mbalimbali
yanayoihusu jamii.
No comments:
Post a Comment