TANGAZO


Monday, March 9, 2015

Burundi:Hussein Rajabu azungumza na BBC

Hussein Rajabu azungumza na BBC
Aliyekuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Hussein Rajabu aliyekuwa ameripotiwa kutoroka jela amemlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa kumpangia njama ya kumfunga jela ilikutokomeza demokrasia nchini humo.
Bwana Rajabu ameiambia BBC kuwa yeye yuko salama na wala hakutoroka jela kama ilivyodhaniwa bali kuwa alitoka jela ''rasmi''baada ya kushirikiana na wafuasi wa chama chake.
Rajabu amesema kuwa wazalendo wenza wa CNDD-FDD ndio walifanikisha kuondoka kwake gerezani kwa ''heshima na taadhima''.
Aidha amemlaumu rais Nkurunziza kwa kukiuka mkataba wa Arusha na badala yake kuunda jopo la wazee aliloliita ''Baraza la Busara'' kwa nia ya kutenganisha viongozi wengine wa chama hicho cha CNDD-FDD
''nimekuwa nikisubiri warundi wenzangu wajadili hili swala wenyewe na pia kwa ushirikiano na viongozi wa mataifa ya kigeni kwa niya ya kutafuta suluahu.''
''kila mtu anajua kuwa sikuwa na hatia yeyote .
''mimi ndiye mwanasiasa aliyepewa adhabu kali zaidi hata ikilinganishwa na watu waliotenda makosa makubwa zaidi ya yangu''
''Ni wazi kuwa ndugu rais Pierre Nkurunziza hakuridhika na majukumu na mapato aliyokuwa nayo na hivyo akanidhulumu'' alisema Bwana rajab.
Hussein Rajabu alikuwa mwanasiasa mashuhuri nchini humo alipohukumiwa kifungo cha miaka 13 jela, mwaka 2007.
Bwana Rajabu alishitakiwa kwa kutaka kuzua vurugu nchini.
Kabla akamatwe mwaka 2007 Hussein Rajabu alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa chama tawala.

No comments:

Post a Comment