Benki kuu ya Uingereza inachunguzwa kuhusiana na vile ilivyotoa fedha za dharura katika mfumo wa benki wa taifa hilo wakati wa msukosuko wa kifedha wa mwaka 2007 na 2008.
Afisi ya kukabiliana na udanganyifu nchini humo itachunguza kile kinachojulikana kama minada ya ukwasi kuona iwapo kuna udanganyifu uliofanywa ili kutoa faida ya wizi.
Mwaka uliopita Benki hiyo ya Uingereza ilichunguza iwapo maafisa wake walijua kuhusu utumiaji m'baya wa soko la fedha za kigeni katika minada hiyo.
Haijulikani ni kwa nini benki hiyo ina wasiwasi,ama iwapo maafisa wake walihusika katika makosa yoyote.
No comments:
Post a Comment