TANGAZO


Wednesday, March 11, 2015

Ajali ya basi na lori maeneo ya Changarawe, mkoani Iringa

Mwenyekiti wa Kamati ya  Usalama  Barabarani Mkoa  wa Iringa  Salim Asas  (kulia ),  akimtazama  mmoja kati ya majeruhi  22  waliolazwa katika  Hospitali ya  Wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa ambao  walipata ajali  mbaya baada ya  basi la majinja lenye namba za usajili T348 CDE kugongana na lori na  kufunikwa na kontena lake jana eneo la Changalawe nje  kidogo ya  mji  wa Mafinga ,katika ajali  hiyo  watu 42  walifariki  dunia (Picha zote na Francis Godwin) 
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  wa  pili kulia akiwa na  viongozi  mbali mbali  wa  tatu ni kamanda  wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi , akifuatiwa na mwenyekiti wakamati ya  usalama barabarani mkoa wa Iringa  Salim Asas na mkuu wa wilaya ya  Mufindi Mboni Mhita  jana walipofika  eneo la  ajali iliyoua 42 na kujeruhi 22.
Basi likiwa limefunikwa na kontena la Lori.
 Basi lililopata ajali likiwa katika eneo la ajali.
Baadhi ya majeruhi wakiwa Hospitali ya Wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa ambao, walipata ajali kupatiwa huduma ya tiba. 
Eneo lililotokea ajali hiyo. 

No comments:

Post a Comment