Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, moja ya kompyuta na baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya dola za Marekani 46,000 vilivyotolewa na WHO kwa Serikali ya Tanzania Dar es Salaam leo, kwa ajili ya maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na ebola.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando wakitiliana saini za makabidhiano ya vifaa hivyo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando wakibadilishana hati baada ya kusaini makabidhiano ya vifaa hivyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando akionesha pampu ya kupulizia dawa kwa mbali za kutibu magonjwa ya kuambukiza.
Wadau wa sekta ya Afya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa vikiwa katika maboksi.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limetoa msaada wa vifaa tiba kwa Serikali ya Tanzania vyenye thamani ya dola la marekani 46,000 kwa ajili ya maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na ebola.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea msaada huo jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando alisema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka wakati serikali ikiwa katika mpango maalumu wa kuiandaa nchi kukabiliana na magonjwa hayo.
"Tunalishukuru shirika la WHO kwa msaada huu mkubwa waliotupatia kwani utatusaidia katika kukabiliana na magonjwa hayo hasa wa ebola ambao umeenea zaidi Afrika Magharibi" alisema Dk.Mmbando.
Alisema ilikukabiliana na changamoto ya magonjwa hayo Serikali imetoa mafunzo, kuimarisha maabara za utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo pamoja na vifaa tiba mbalimbali.
Alisema utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo vinafanyika katika maabara kubwa iliyopo katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya pamoja na Muhimbili.
Dk. Mmbando alisema tangu ugonjwa huo uibuke katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi umewaathiri watu 23,000 pamoja na kusababisha vifo vya watu 9,000.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO), Rutaro Chatora alisema shirika hilo limekuwa likisaidia misaada ya huduma za afya katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi za Guinea, Liberia na Siera Leon.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment