TANGAZO


Sunday, February 15, 2015

Wenger:Sanchez ana ishara za uchovu

Alexi Sanchez
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba mshambuliaji wake nyota Alexi Sanchez huenda ameanza kuonyesha ishara za uchovu.
Mchezaji huyo wa taifa la Chile amefunga mabao 18 katika mechi 32 za the Gunners ,lakini Wenger anahisi kwamba Sanchez hakucheza vyema wakati wa mechi ya ushindi dhidi ya Leicester.
Sanchez alipata jereha la mguu na hivyobasi kutolewa wakati wa mechi hiyo na sasa haijulikani iwapo atacheza mechi ya FA siku ya jumapili dhidi ya Middlesbrough.
''Hakucheza kama anavyocheza kila siku'',.alisema Wenger.

No comments:

Post a Comment