TANGAZO


Wednesday, February 25, 2015

Waislamu taabani, Austria Kunani ?

Bunge la Austria lajiandaa kujadili mswada utakaowanyima waislamu uhuru wa kupokea msaada wa kimataifa
Bunge la Austria linajiandaa kujadili mabadiliko yenye utata kuhusiana na sheria dhidi ya Uislamu.
Sheria hiyo mpya itazuia ufadhili wa kifedha kutoka mataifa ya nje katika ujenzi wa misikiti .
Ufufuaji wa sheria hiyo iliyodumu nchini humo kwa kipindi cha karne moja iliyopita utawaruhusu wakristu na wayahudi kupata ufadhili kutoka mataifa ya kigeni ilahali inawanyima waislamu uhuru wa kupokea msaada kutoka
ughaibuni.
Wakristu na wayahudi wataruhusiwa kupokea misaada iwapo sheria hiyo itapitishwa lakini Waislamu na Masheikh hawatoruhusiwa
Kwa mujibu wa waziri wa mtagusano na umoja wa taifa, Sebastian Kurz, sheria hiyo inalenga kuilinda mtagusano wa taifa japo viongozi wa Kiislamu wamepinga vikali mswada huo wakisema utawabagua.
Bwana Kurz amesema wazo la kubadilisha sheria hiyo limetokana na mashambulizi yaliyotokea huko Ufaransa na Denmark.
Aidha mapumziko ya siku zao takatifu kutoka kazini bila ya kupewa adhabu na pia kupata muongozo wa kiroho katika taasisi kadha za serikali kama vile magereza na hospitalini.

No comments:

Post a Comment