Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo Bw. Moshi Hussen (wa kwanza kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Ofisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga(wa kwanza kulia) walipofika ofisini kwake leo kwa ajili ya kujitabulisha kabla ya kuanza utekelezaji wa ziara yao wilayani humo. Kutoka kushoto kwa Kaimu Katibu Tawala ni Afisa Vijana wa Wilaya ya Kibondo Bi. Safi Mtula, Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurian Masele na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibondo Bw. Abel Nuba .
Ofisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwasilisha mada kuhusu mwongozo wa mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kibondo katika warsha iliyoandalliwa na Wizara hiyo na kushirikisha jumla ya Vijana 83 kutoka katika Halmashauri za Kibondo na Kakonko.
Baadhi ya Vijana kutoka Wilaya za Kibondo na Kakonko
wakifuatilia mada zilizokuwa zina wasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) wakati wa mafunzo kuhusu
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Uongozi Bora na Sera ya Maendeleo
ya Vijana leo wilayani Kibondo.(Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
No comments:
Post a Comment