Kiongozi Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, akizungumza katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kushoto ni Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo, Buguruni, Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakichukua habari kwenye mkutano huo, Buguruni, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakichukua habari kwenye mkutano huo, Buguruni, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emmanuel Makaidi, akizungumza kwenye mkutano huo, huku akiishangaa Serikali kwa kile alichodai kutokushughulikia masuala ya wananchi na badala yake kushughulikia masuala ya kura ya maoni kuhusu Katiba inayopendekezwa.
Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo, Buguruni, Dar es Salaam leo.
Na Suleiman Msuya
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameitaka Serikali kuacha kuipelekesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili iweze kukamilisha mchakato wa kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kumaliza uongozi wake kwa amani kwani dalili zinazoenekana za kulazimisha mchakato huo ni ishara tosha ya kusababsha upotevu wa amani nchini.
Pia wameitaka NEC iache kutumika kwani kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria mbayo imewezesha ofisi hiyo kuwepo.
Hayo yamesemwa na viongozi wa Ukawa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano huo ambao ulifanyika makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa Freeman Mbowe alisema haipo sababu ya Serikali kulazimisha suala hilo kwani halitakuwa na tija kwa Taifa.
Mbowe alisema zipo taarifa ambazo zinasambwa kuwa NEC inalazimishwa kukamisha mchakato huo ili kura ya maoni iweze kufanyika mwezi Aprili jambo ambali halikubaliki na haliwezekani.
Alisema hadi sasa vifaa vyote vinavyohusika havijafika nchini hivyo tume kuendelea kuwadanganya wananchi kuwa mchakato huo unaenda vizuzi ni kupotosha umma.
Mwenyekitin huyo Mwenza alisema wao wataendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa lengo la uchaguzi ujao ila msimamo wao wa kutoshiriki kura ya maoni upo pale pale.
"Unajua nasdindwa kuelewa ni kwa nini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inashabikia kura ya maoni katika jambo la haramu kama hilo la Katiba iliyopendekezwa jambo ambalo linasababisha NEC kufanya kazi kwa hofu kubwa," alisema Mbowe.
Mbowe alisema baada ya kutafakari ukimya wa CCM wanapata shaka kuwa kuna msukumo kutoka katika chama na Serikali kwani pamoja na mapungufu yote ambayo yanabainika CCM imekaa kimya.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CUF ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa Profesa Ibrahim Lipumba alimtaka Rais Kikwete kumaliza uongozi wake kwa amani kwani hakuna sababu ya kulazimisha jambo ambalo halina tija.
Lipumba alisema mchakato huo umegubikwa na kasoro nyingi hivyo kunahitajika busara pekee ili kuhakikisha kuwa hakuna tofauti ambazo zinatokea kupitia uandikishwaji wa daftari la kudumu.
Pro. Lipumba alisema NEC inakabiliwa na changamoto nyingi za kifedha wataalam na mahitaji mengine hivyo ni jambo la aibu kuhakikishia Watanzania kuwa kuna muafaka utafikiwa katika mchakato huo.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha National League Democratic Dk. Emmanuael Makaidi alisema ni vyema Rais kutambua kuwa historia za uongozi hailazimishwi, hivyo kumtaka kutambua kuwa hicho alichokifanya katika suala la katiba linatosha.
Makaidi alisema iwapo atataka kujenga historia ambayo haina faida na wananchi ni kuendelea kulazimisha mchakato huo ambao kwa mtazamo wake ni haramu kwa jamii ya Watanzania.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Mosena Nyambabe alitoa wito kwa NEC kutoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo wa daftari la kudumu la wapiga kura kwani ni dhahiri kila mtu yupo njia panda ya ni wapi kutafuata baada ya Njombe.

No comments:
Post a Comment