TANGAZO


Wednesday, February 25, 2015

Redd's Miss Tanzania Namba Tatu 2014, Doris Moleli kugawa vitabu kwa Shule 3 za Msingi mkoani Singida

Redd's Miss Tanzania namba tatu 2014, Doris Mollel akimsikiliza Ofisa Taarifa wa Mradi wa Vitabu vya Watoto wa Childrens Book Project for Tanzania (CBP), Ramadhan Ally, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitabu 200, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuvigawa kwenye Shule 3 za Msingi za Munguli, Kindai na Midamigha zote za mkoani Singida.
Redd's Miss Tanzania namba tatu 2014, Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na Ofisa Taarifa wa Mradi wa vitabu vya watoto Childrens Book Project for Tanzania (CBP), Ramadhan Ally, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuvigawa kwenye Shule 3 za Msingi za Munguli, Kindai na Midamigha zote za mkoani Singida. (Picha zote na Albert Manifester)

Na Suleiman Msuya
MISS Tanzania Namba Tatu Doris Moleli anatarajia kutoa vitabu 200 katika Shule 3 za Msingi za Munguli, Kindai na Midamigha mkoani Singida mwezi ujao.

Moleli alisema lengo la kutoa vitabub hivyo, ni katika mkakati wake wa kusaidiana na Serikaki kuboresha Elimu ya Msingi Tanzania.
Miss Tanzania huyo namba tatu, ambaye pia Miss Kanda ya Kati alisema vitabu hivi vimetolewa na Children’s Book Project for Tanzania na vinalenga maelfu ya watoto nchini katika kuwakomboa kielimu.
"Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi yakunufaika zaidi kielimu," alisema Moleli. 

Tafiti mbalimbali kutoka serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo za mtoto. 
Elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadaye.
Kwa upande wake Ofisa Taarifa wa Programu ya Children's Book Project For Tanzania  alisema vitabu hivyo vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku.

"Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu," alisema Ally. 

Alisema taarifa zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika. 

No comments:

Post a Comment