Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipofika kutoa pole kwa kizuka wa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo. (Picha zote na Ikulu)
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawaker na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed (katikati) pamoja na wake wa Makamo wa Pili wa Rais na Kinamama wakijumuika kwa pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo.
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali kike kwa kiume walijumuika pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika kutoa pole Nyumbani kwa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Magomeni Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine walipofika kutoa pole kwa wafiwa Nyumbani kwa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Magomeni Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja Viongozi mbali mbali walijumika pamoja katika kumswalia Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) katika masjid Nuru Muhammad Mendae Mjini Unguja leo Swala iliyoongozwa Kadhi Mkuu na Sheikh Khamis Haji na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguuja.
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali Bara na Visiwani wakilibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) wakati wa maziko yaliyofanyika leo Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) pamoja Viongozi mbali mbali walijumika na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Marehemu Salmin Awadh aliyezikwa kijijini kwao Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali wa Mjini na Mashamba walijumuika kwa pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) yaliyofanyika leo Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitia udongo wakati alipojumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakati wa maziko ya aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Marehemu Salmin Awadh aliyezikwa kijijini kwao Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
No comments:
Post a Comment