Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Glee Magembe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya baraza hilo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza, Daniel Mafie, Afisa Habari wa MAELEZO, Frank Mvungi na Afisa Habari wa NECTA, John Nchimbi.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano kati ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo.
Frank Mvungi-Maelezo
BARAZA la Mitihani
Tanzania (NECTA) kwa kushirikiana na Kamati za Uendeshaji Mitihani za mikoa na
wialaya limefanikiwa kudhibiti na kuondoa tatizo la wizi wa mitihani katika
mitihani ya Taifa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa
Idara ya Utawala na Fedha wa NECTA, Daniel Mafie
wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo.
Mafie amesema pamoja na kudhibiti wizi huo, pia
NECTA limefanikiwa pia kudhibirti udanganyifu wakai wa ufanyaji wa mitihani ya
Taifa.
Alisema katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi udanganyifu
umepungua kutoka watahiniwa 9,736 mwaka (2011) hadi 293 mwaka 2012.
Kwa Mwaka 2013 udanganyifu umepungua kutoka
watahiniwa 13 hadi 01 mwaka 2014 hali inayoonyesha kuwa tatizo hilo
limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.
“Katika mtihani wa kidato cha nne (CSEE) udanganyifu
umepungua kutoka watahiniwa 3,303 (2011), hadi 789 mwaka 2012” alisema Mafie.
Aidha katika Mtihani wa kidato cha Sita (ACSEE)Mafie
alibainisha kuwa udanganyifu umepungua kutoka watahiniwa 11 mwaka 2011 hadi 6
mwaka 2012,wakati mwaka 2013 watahiniwa waliofanya udanganyifu walikuwa 4 na
kupungua hadi 3 mwaka 2014.
Katika kuboresha huduma zinazotolewa na NECTA, Mafie
alibainisha kuwa Baraza hilo limeanzisha utaratibu wa kutoa matokeo ya mitihani
kwa njia ya mtandao wa simu ambapo unatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneo (SMS)
ambao ni gharama nafuu.
Ujumbe huo unatumwa kwenda namba 15311 ambapo
mtahiniwa anatuma neno Matokeo* namba ya
shule/kituo*namba ya mtahiniwa*aina ya mtihani *mwaka mtihani ulipofanyika, na
baada ya hapo atapokea matokea yake.
Alisema kujua nafasi ya shule
Kitaifa,Mkoa,Halmashauri andika neon rank * namba ya shule/kituo* aina ya
mtihani* na mwaka mtihani ulipofanyika.
Suala la wizi wa mitihani ya Taifa na udanganyifu
katika mitihani hiyo, limekuwa moja ya mambo yanayolikabili baraza hilo katika
miaka ya hivi karibuni.
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni Taasisi ya
Umma chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa ajili ya
kuendesha Mitihani ya Taifa.
NECTA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.21 ya mwaka
1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002.





No comments:
Post a Comment