Mamia ya waombolezaji wakiwawamebeba jeneza lililokuwa na mwili aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba na Taifa Stars Marehemu Christopher Alex, wakati akienda kuuzika katika Makaburi ya Nkhungu Dodoma leo. (Picha zote na John Banda-Dodoma)
Mtoto wa marehemu Christopher Alex, Asnat Christopher akilia kwa uchungu wakati alipokuwa akipita mbele ya jeneza la marehemu Baba yake, wakati wa kuuaga mwili huo.
wachezaji wa kizazi cha Dhahabu, waliopata kuwika miaka ya 2003 pamoja na Marehemu Christopher Alex Masawe, Ulimboka Mwakingwe, Juma kaseja, Bonface Pawassa na Aman Mbaruku, wakipita mbele ya sanduku lililokuwa na
mwili wa marehemu Christopher Alex kabla ya mazishi yaliyofanyika katika Makaburi ya Nkhungu Dodoma leo.
Mchezaji wa zamani ya CDA ya Dodoma, Juma Ikaba, Juma Kaseja (katikati), aliyewahi kuichezea timu ya Simba na Meneja wa Timu ya Polisi Dodoma, wakite jambo walipokuwa katika msiba wa marehemu Christopher Alex aliyezikwa leo, mjini Dodoma.
Juma Kaseja (katikati mwenye fulana nyekundu), ambaye leo, amegeuka kituko kwa kukataa kumshika mkono mama yake marehemu Alex, huku akiwa amevalia kofia upande na kusababisha miguno toka kwa waombolezaji, wakati mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba miaka ya 2003, ulipokuwa ukiagwa nyumbani kwa mama yake, Bandeko, mjini Dodoma, akiwa na Ulimboka Mwakingwe, Bonface Pawasa na Amani Simba.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Ally Sullu akipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Christopher Alex, kabla ya mazishi mjini Dodoma leo.
Mchezaji wa zamani wa Simba Amani Mbaruku akimnyamazisha mchezaji waliocheza naye miaka hiyo ya 2003, Boniface Pawasa, aliyeshindwa kujizuia kwenye msiba wa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Christopher Alex.
Boniface Pawasa akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Simba, Christopher Alex.
Boniface Pawasa akirekebisha jeneza lenye mwili wa merehemu Christopher Alex, waliyecheza pamoja miaka ya 2003 kwenye Klabu ya Simba ya Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment