TANGAZO


Monday, February 2, 2015

Mbunge Hamad Rashid awaasa wanafunzi wa CBE kujiunga na Mfuko wa PSPF ili kupata mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha


Mgeni rasmi, Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), akizunguza na wanafunzi walioudhuria kwenye siku ya Career Day, iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha Biashara,(CBE), Ramadhani S Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY", iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Ofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Hadji Jamadary akifafanua jambo na kuelezea kuhusu uchangiaji wa hiari wa mfuko wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Maseko Kodalo, Ofisa wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, akitoa maelekezo kuhusu kujiunga na mfuko huo, kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha.
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba, kupitia Chama cha CUF akipewa ufafanuzi kuhusu kazi za mfuko wa PSPF na Ofisa wa PSPF, Hadji Jamadary (wa pili kutoka kushoto).
Mbunge wa Jimbo la Wawi kisiwani Pemba, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mh. Hamad Rashid akiwa ndani ya banda la PSPF, ambao walikuwa wadhamini wakuu katika maadhimisho ya Career Day.
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF, akipata ufafanuzi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu ya Biashara (CBE) wa kozi mbalimbali kuhusu kazi zao na maendeleo ya masomo yao.
Ofisa wa PSPF, Hadji Jamadary akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda la mfuko wa PSPF.
Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Mfuko wa PSPF wakipatiwa elemu kuhusu mikopo ya kuanzia maisha na fao la elimu.
Ofisa wa  mfuko wa Pesheni (PSPF), Abdallah Ahamed akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanachuo, waliotembelea kwenye banda la PSPF.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), jijini Dar es Salaam, wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF.
Baadhi ya washiriki wa Cereer Day, wakiwa katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi walioweza kutembelea banda la PSPF, na kuweza kuelimishwa juu ya fao la elimu na mikopo ya kuanzia maisha, wakitizama mtandao wa Mfuko huo kwa njia ya simu.
Mgeni Rasmi na wafanyakazi wa PSPF, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Biashara (CBE),  jijini Dar.

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Wawi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mh. Hamad Rashid Mohamed, ameupongeza mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kuwa wadhamini katika Career Day ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho,  siku ya Ijumaa.
Mbunge huyo, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo, alitoa pongezi hizo kwa PSPF kwa kitendo cha kuweza kuwa pamoja na wanafunzi kwa ajili ya kuwaandaa kuwa washiriki wazuri katika uchangiaji wa mafao mbalimbali na kuweza kupata mikopo ya elimu na ile ya kuanzia maishi.

Awali akizungumza Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara (CBE), Bw. Ramadhani S Kirungi amewashukuru wanafunzi wote, walio weza kushiriki katika sherehe hizo, kwani ni za kwanza toka chuo hicho kianze, yapata miaka hamsini (50), hazijawahi fanyika na kuongeza kwamba uongozi wake amepata bahati ya kuweza kuifanya siku hiyo.
Pia amewapongeza wanafunzi wa kozi mbalimbali walio weza kufanya maonesho katika viwanja vya chuo hicho kwaajili ya kuwaonesha wahudhuriaji ufasaha wa masomo yao.
Mfuko wa Pensheni wa  PSPF kupitia Maafisa wao walio weza kujitoa kwa ajiri ya kuwapa elimu ya jinsi na namna ya kujiunga na mfuko huo hususani katika fao la elimu na fao la kuanzia maisha ambapo ni mfuko mojawapo wenye manufaa makubwa kuliko mifuko mingine unaoweza kutoa huduma kulingana na mahitaji wa watanzania pasipo na ubaguzi wala upendeleo.
Maseko Kodalo Ambaye ni Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF yeye aliweza kutoa rai kwa wanafunzi wote na wananchi wote waweze kujiunga na mfuko huo ili kuweza kupata mafanikio, alitoa mifano michache ambayo inawezekana ukaimudu pindi unapo jiunga na mfuko huo ambapo kwa mwanafunzi alitaja kuwa unaweza kupata mikopo na kujiwekea akiba ili kuweza kukusaidia katika masomo, vilevile kuna mikopo ya kuanzia maisha  ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wanyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama .

No comments:

Post a Comment