TANGAZO


Saturday, February 14, 2015

Matokeo Kidato cha Nne 2014 yatolewa

Katibu wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne na QT kwa mwaka 2014.

Na Celina Mathew
WASICHANA wamendelea kutamba matokeo kidato cha nne ya mwaka 2014 ambapo nafasi ya kwanza Kimkoa imeshikwa na Nyakaho Marungu wa Shule ya Sekondari Baobab iliyopo mkoani Pwani.
Aidha shule iliyoshika nafasi ya kwanza, katika kumi bora ni Kaizirege, iliyopo Kagera huku nafasi ya mwisho ikishikiliwa na Magoma iliyopo Mkoa wa Tanga.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Musonde alisema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 12.67 kutoka asilimia 57.09 kwa mwaka 2013 hadi asilimia 69.76 kwa mwaka jana.


Alisema kupanda kwa ufaulu huo kwa mwaka huu kumetokana na jitihada zilizofanywa na Serikali katika kuboresha elimu nchini kupitioa mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN).


Aidha, Mpango huo wa Serikali wa kuimarisha tathimini ya elimu kwenye mtihani wa kidato cha pili za kuweka utaratibu wa kubaini wanafunzi wenye alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu umeonesha kuwaimarisha zaidi wanafunzi katika kumudu masomo yao na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri zaidi wanapofika kidato cha nne.


Msonde alisema pamoja na kupanda kwa ufaulu wa jumla, takwimu zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo yaliyomengi upo chini ya asilimia 50 hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo yote ikiwa ni pamoja kuongeza idadi ya watahiniwa kwenye madaraja ya juu ya ufaulu.

Alisema jumla ya watahiniwa 196,805 sawa na asilimia 68.33 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefaulu ambapo wasichana waliofaulu ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85.
Musonde alisema mwaka 2013 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 235,227 sawa na asilimia 58.25 hivyo ufaulu umepanda kwa asilimia 10.08 ikilinganishwa na mwaka huo.

Alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani ambapo wasichana ni 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana ni 91,693 sawa na asilimia 70.67.

"Mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule waliofaulu mtihani huo. hivyo ufaulu wa watahiniwa wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013, "alisema.

Akizungumzai kuhusu watahiniwa wa kujitegemea alisema idadi ya watahiwa waliofaulu mtihani ni 29,162 sawa na asilimia 61.12. mwaka jana watahiniwa walikuwa 34,075 sawa na asilimia 66.3 waliofaulu mtihani huo.

Kwa upande wa watahiniwa wa mtihani wa marifa (QT) alisema idadi ya watahiniwa wa mtihani huo, waliofaulu ni 6,810 sawa na asilimia 55.29. kwa mwaka 2013, watahiniwa walikuwa 6,59 sawa na asilimia 43.38 walifaulu mtihani huo.

Akizungumzia ubora wa ufaulu alisema kwa kuangalia madaraja unaonesha kluwa watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merits na Credt katika mwaka 2014 ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana 45,841 sawa na asilimia 35.33.


Kwa upande wa ufaulu wa wataniwa wa shule katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013 ambapo ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wa shule waliofanya somo hilo wamefaulu.


Alisema ufaulu wa chini kabisa ni ule wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58 ya watahiniwa wote wa shule waliofanya somo hilo wamefaulu huku masomo ya sayansi (Physics, Chemistry na Biology) umeendelea kuimarika kidogo kwa kulinganisha na ufaulu wa masomo hayo kwa mwaka 2013.


Kwa upande wa upangaji wa shule kwa ubora wa ufaulu alisema umetumia kigezo cha wastani wa pointi (Grade Point Average), katika ufaulu wa masomo watahuiniwa katika shule, ambapo A=5, B+=4, B=3, C=2, D=1 na E=0.5.

Alizitaja shule kumi bora kuwa ni Kaizirege ilityopo (Kagera), Mwanza Allience (Mwanza), Marian Boys (Pwani), St. Francis Girls (Mbeya), Abbey (Mtwara), Feza Girls (Dar es Salaam), Cannosa (Dar es Salaam), Bethel Sabs Girls (Iringa), Marian Girls (Pwani) na Feza Boys (Dar es Salaam).

Aliongeza shule kumi bora za mwisho ni Manolo iliyopo Mkoani Tanga, Chokocho (Pemba), Kwaluguru (Tanga), Relini (Dar es Salaam), Mashindei (Tanga), Njelekela Islamic seminary (Kigoma), Vudee (Kilimanjaro), Mnazi (Tanga), Ruhembe (Morogoro0 na Magoma (Tanga).


Aidha Msonde alitaja watahiniwa kumi bora kitaifa kuwa ni Nyakato Marungu wa Baobab (Pwani), Eltoni Jacob wa Feza Boys (Dar es Salaam), Samwel Adam wa Marian Boys (Pwani), Fairness Mwakisimba wa St. Fransis Girls (Mbeya), Mugisha Lukambuzi wa Bendel Memorial (Kilimanjaro).


Wengine ni Paul Jijimya wa Marian Boys (Pwani), Angel Mcharo wa St. Francis Girls (Mbeya), Atuganile Jimmy wa Cannosa (Dar es Salaam), Jenifa Mcharo wa St. Francis Girls (Mbeya) na Mahmoud Bakili wa Feza Boys (Dar es Salaam).


Msonde alitaja wasichana kumi bora kitaifa kuwa ni Nyakaho Marungu wa Baobab (Pwani), Fairness Mwakisimba wa St. Fransis Girls (Mbeya),Angel Mcharo wa St. Francis Girls (Mbeya), Atuganile Jimmy wa Cannosa (Dar es Salaam).


Wengine ni Jenifa Mcharo wa St. Francis Girls (Mbeya), Levina Ndamugoba wa Msalato (Dodoma), Veronica Wambura wa Cannosa (Dar es Salaam), Sifaely Mtaita wa St. Mary's (Tanga), Catherine Ritte wa St. Francis Girl's (Tanga) na Anastazia Kabalinde wa Kaizigere (Kagera).


Aidha wanaume kumi bora ni Eltoni Jacob wa Feza Boys (Dar es Salaam),Samwel Adam wa Marian Boys (Pwani),Mugisha Lukambuzi wa Bendel Memorial (Kilimanjaro), Paul Jijimya wa Marian Boys (Pwani), Mahmoud Bakili wa Feza Boys (Dar es Salaam).

Wengine ni Amani Andrea wa Moshi Technical(Kilimanjaro), Mahmoud Msangi wa Feza Boy's(Dar es Salaam), Haji Gonga wa feza Boys (Dar es Salaam) na Kelvin Sessan wa Feza Boy's (Dar es Salaam).
Aidha baraza hilo limezuia kutoa matokeo ya watahiwa 42 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo.

"Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu,"alisema.


Pia watahiniwa 47 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote wamepewa fursa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka huu.


Wkati huohuo baraza hilo limewafutia matokeo watahiniwa 184 waliobainika kufanya udanganyifu ambapo 128 ni wakujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.

Aidha vituo viwili vya watahiniwa wa kujitegemea ambavyo ni P2617 Kisesa na P4806 Ubango ndivyo vilivyokiuka taratibu za ufanyikaji wa mtihani wa kuruhusu udanganyifu kufanyika.

Msonde alisema kutokana udanganyifu huo anazitaka mamlaka husika ziwachukuliwe hatua za kibinadamu wasimamizi waliosimamia mitihani katika vituo hivyo kwa mujibu wa kanuni za utumishi.

Aliongeza kuwa kwa mwaka huu hakuna wanafunzi waliochora nyimbo kwenye karatasi za mitihani tofauti na siku za nyuma hali inayoonesha kuwa wanafunzi wameimarika vya kutosha katika kujibu mitihani yao kwa umakini.

No comments:

Post a Comment