TANGAZO


Tuesday, February 17, 2015

Maafisa Polisi 20 wauawa Afghanistan

Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakihatarisha usalama wa Afghanistan
Maafisa Mashariki mwa Afghanistan wamesema maafisa wa Polisi 20 wameuawa katika mashambulio kadhaa.Watu wanne wameripotiwa kuvalia mavazi ya Polisi na kuingia katika Ofisi za makao makuu ya Polisi katika jimbo la Logar, na kujilipua.
Gavana wa Jimbo hilo Niaz Muhammad Amiri ameiambia BBC kuwa Maafisa wengine wanane walijeruhiwa.Wengi kati ya waliopoteza maisha walikuwa wakipata chakuwa wakati wa mapumziko.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya Wanamgambo miezi ya hivi karibuni wakati ambapo vikosi vya usalama vikiwa vimechukua udhibiti wa nchi hiyo kutoka kwa Majeshi ya NATO.

No comments:

Post a Comment