TANGAZO


Thursday, February 19, 2015

"Hakuna Wasichoweza", Mradi unaoleta matumaini mapya kwa watoto wa kike mashuleni

*Umeonyesha mafanikio kwa muda mfupi mkoani Lindi na Mtwara
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi  wakimsikiliza kwa makini mwalimu wa masuala ya Afya na Uzazi  wa Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi, mpango huu uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara
Wasichana kutoka kata ya Ufukoni mkoani Mtwara wakisubiri kupatiwa pedi kwa ajili ya kujisitili kipindi wakiwa kwenye hedhi na kupatiwa elimu ya Afya na uzazi chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation.Mradi huo unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wale wasio mashuleni ambapo zoezi hili limeanza kufanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi  wakifurahia baada ya kugawia pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye hedhi .Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi  wakifurahia baada ya kugawia pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye hedhi .Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi  wakifurahia baada ya kugawia pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye hedhi .Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara.

Na Mwandishi wetu
SASA nafurahia masomo yangu ikiwemo maendeleo yangu darasani kuwa mazuri darasani.Najisikia vizuri kuwa mwanafunzi. 
Natamani mradi wa Hakuna Wasichoweza  ungeanza kitambo.Hata  hivyo naona mabadiliko makubwa ya kumuwezesha mtoto wa kike na kumjengea uwezo wa kujiamini yanakuja tukiendelea na kasi hii…”

Haya yalisemwa na Sharifa Hamis, mmoja wa wanafunzi wa sekondari mkoani ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Mtwara wakati akitoa ushuhuda kwa niaba ya wenzake ni kwa jinsi gani  wasichana wenzake zaidi ya 5,000 wamenufaika na mradi alipohojiwa hivi karibuni.

Mwanafunzi Sharifa alikiri kuwa tangu kuanzishwa kwa mradi wa Hakuna Wasichoweza maarufu kama Girl Power mahudhurio ya wasichana shuleni kipindi chote cha masomo yameongezeka pia ufanisi wao katika masomo umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.Ushuhuda huo uliungwa mkono na mwalimu Masoud Issa anayefundisha katika shule hiyo.

Baada ya kupatiwa mafunzo ya Afya na  mafunzo kuhusiana na  mabadiliko ya miili yao ikiwemo kuwapatia pedi wasichana wanaotoka katika familia maskini kwa ajili ya kujihifadhi wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi wasichana wengi wameanza kujiamini na kupunguza utoro wa kuja shuleni uliosababishwa na hali hiyo kutokana na shule wanazosoma kutokuwa na mazingira rafiki ya kujihifadhi katika kipindi hicho.

Mafunzo  kwa wasichana na namna na kujihifadhi wakati wakiwa hedhi pamoja na afya ya uzazi yanafanyika chini ya uwezeshaji wa walimu na wauguzi waliopewa mafunzo hayo. Kitini cha kufundishia juu ya masuala haya kimeweza kuandaliwa na taasisi ya T-MARC kwa kushirikiana  na Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia mradi huu wa ‘Hakuna Wasichoweza’ na kina maelezo ya kina juu ya umuhimu wa afya,elimu ya uzazi na  matumizi ya Pedi.

Mmoja wa walimu wanaotoa mafunzo kwa wasichana Monica Mfaume,anasema kuwa mradi huu umeleta mabadiliko makubwa katika kipindi cha muda mfupi tangu uanze na aliwapongeza waliounzisha na kuwaomba waufanye kuwa endelevu na  usambae nchi nzima na kuwafikia wasichana wengi zaidi. “Tatizo la mahudhurio hafifu ya wasichana na kufanya vibaya katika masomo ikiwemo kupata mimba katika umri mdogo kutokana na kutojua mabadiliko katika makuzi yao lilikuwa linatuvunja moyo lakini angalau hivi sasa linapungua kwa kasi eneo hili la mradi ”.Alisema
Meneja Uhusiano wa taasisi ya T-MARC inayotekeleza mradi chini ya  ufadhili wa USAID na Vodacom Foundation,Maurice Chirimi, anasema kuwa mradi umeonyesha kuwa na mafanikio kwa muda mfupi wa miaka 2 ya awamu ya kwanza kwa  mafunzo pamoja na pedi za bure  kuwafikia wasichana  zaidi ya 5,232 waliopo katika shule 24 za msingi na wengine 552 wasiokuwepo mashuleni katika kata 17 mkoani Mtwara.

Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza  ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi watoto wa kike zaidi ya wasichana 10,000 waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mtwara na Lindi.Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume.

Nia ya Hakuna Wasichoweza  ni  kuwaona walimu ,watoto wa kike na  wanajamii kwa ujumla ikiwemo wanaharakati wa masuala ya elimu wakiunga mkono juhudi hizi ili kwa pamoja tuifikie dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2015.Elimu Bora bila ubaguzi inawezekana,Timiza wajibu wako.

No comments:

Post a Comment