TANGAZO


Monday, February 16, 2015

Ebola:Shule zafunguliwa Liberia

Shule zafunguliwa tena huko Liberia
Kuanzia leo shule nchini Liberia zinaendelea kutoa mafunzo baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa Ebola.
Huku kukiwepo vifo vya karibu watu 4000, Liberia imekuwa nchi iliyoathirika zaidi katika nchi tatu zilizogubikwa na janga hilo,
lakini wiki kadhaa zilizopita maafisa wa serikali wameamua kwamba kupungua kwa visa vipya vya maambukizi kunatoa nafasi ya kufunguliwa upya shule hizo.
Lakini wakati watoto wengi wanaelekea madarasani, hatua za kiafya zilizochukuiwa kudhibiti ugonjwa huo zimesababisha baadhi ya wanafunzi kutojumuika na wenzao kwa mafunzo.
Shule zimefunguliwa tena nchini Liberia, baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Muhula mpya umeanza rasmi siku moja tu baada ya marais wa Liberia na Sierra Leone, kufanya ziara ya kwanza katika nchi za ngambo.
Wanafunzi wakisaidia kufyeka nyasi shuleni katika siku yao ya kwanza
Wawili hao walihudhuria mkutano wa kimataifa nchini Guinea ambako waliapa kutokomeza ugonjwa huo kufikia aprili mwaka huu.
Afisa mmoja wa shirika la umoja wa mataifa la masuala ya watoto UNICEF amesema kuwa wanafunzi wengi wamerejea shuleni mapema hii leo na alishuhudia jinsi waalimu katika shule kadhaa wanavyochukua hatua za tahadhari.
Wanafunzi walilazimishwa kunawa mikono yao kabla ya kuingia darasani huku viwango vya joto vikichukuliwa kutoka kwa kila mwanafunzi.
Waalimu pia waliwaeleza wanafunzi jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo wa ebola.
Shirika la UNICEF limekuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kuhusiana na mbinu za kuzuia ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tisa katika mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Rais wa Guinea Alpha Conde , Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Ernest Bai Koroma wa Sierra leone, wameungana pamoja na kutoa taarifa ya pamoja wakisema nia yao ni kutokomowza ugonjwa huo katika kipindi cha siku sitini.
Hata hivyo, kumekuwa na visa vipya vya maambukizi nchini Guinea katika siku za hivi karibuni.
Walimu wakiwapokea wanafunzi baada ya kufungwa shule kwa muda mrefu
Mwezi huu pekee watu sitini walipatikana na virusi vya ebola, na nchini Sierra Leone shirika la afya duniani limesema watu sabini na sita waliambukizwa.
Liberia ndio nchi iliyoshuhudia visa vingi vya ugonjwa huo na ndio nchi iliyoadhirika zaidi.
Shirika la UNICEF na mashirika mengine yametoa vifaa elfu saba mia mbili vitakavyotumika katika shule elfu nne nchini Liberia.
Zaidi ya waalimu elfu kumi na tano na wakuu wa shule mbali mbali nchini humo pia wamefunzwa mbinu
za kuzuia na kujikinga kutoka na virusi vya Ebola.
Katika nchi jiranai ya Guinea zaidi ya watoto milioni moja nukta tatu wamerejea shuleni hii leo.

No comments:

Post a Comment