Baada ya kuanza vema mechi zao za michuano ya vilabu barani Afrika, makocha wa wawakilishi wa Tanzania, Azam FC na Yanga wamesema kuwa wana matumaini ya kusonga mbele katika mechi zao za marudiano zitakazofanyika baada ya wiki mbili mjini Khartoum (Sudan) na Gaborone (Botswana).
Yanga, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) waliwafunga BDF XI ya Botswana 2-0 na kocha wa Yanga, Mdachi Hans Van de Pluijm amesema amefurahishwa na ushindi huo na kusema anahitaji goli moja tu au zaidi katika mechi ijayo ili timu yake isonge mbele.
“Tunahitaji ushindi mdogo au sare ya kutokufungana ili tusonge mbele”,
“Tumeweza kuutumia vyema uwanja wa nyumbani na tunahitaji ushindi mwingine ili tufanikiwe”, alisema Pluijm, huku amkimsifia Mrundi Amisi Tambwe kwa kufunga magoli yote.
Naye kocha wa Azam, Mcameroon, Joseph Omog amekisifu kikosi chake kwa kuwafunga El-Merreikh ya Sudan 2-0.
“Tunakazi ngumu mechi ya marudiano kwa kuwa wapinzani wetu ni wazuri na watakuwa wakicheza nyumbani, ila tunajitahidi ili tuweze kufunga zaidi ili tusonge mbele.
Azam ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga, iliyofikisha miaka 80 mwezi Februari mwaka huu tangu ilipoanzisha, ikiwa na uzoefu wa kutosha.
No comments:
Post a Comment