Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao (kushoto), akihakiki namba ya simu ya mshindi wa promosheni ya JayMillions anayoonyeshwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati), wakati wa kuchezesha droo ya 13 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Mkazi wa Magu James Mangu amejishindia kitita cha shilingi Milioni 10/- anaeshuhudia kulia ni Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati), akiongea na mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya JayMillions Mkazi wa Magu mkoani Mwanza James Mangu.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Na Mwandishi Wetu
Januari 28,2015
Januari 28,2015
MKAZI wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza James Mangu, leo ameibuka mshindi wa shilingi milioni 10 katika droo ya kumi tatu ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mangu ambaye ni baba mwenye watoto 4 ambaye pia ni mjasirimali amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa katika kazi zake za biashara na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.
“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na biashara na kukumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa mtaji.Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya kuuza dawa za binadamu biashara ambayo nilikuwa naota kuifanya kwa muda mrefu”.Alisema Mangu kwa furaha.
Mbali na kuanzisha biashara amesema fedha zake zitamsaidia kulipia watoto wake ada za shule ikiwemo kuboresha makazi yake “.Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu.
Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.
Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-.
Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari mteja 1 mkazi wa mkoa Katavi,Hynes Kanumba,amekwishajishindia milioni 1 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na tatu hivyo bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.
Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.
Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.
Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-




No comments:
Post a Comment