TANGAZO


Friday, January 30, 2015

BUNGE LEO DODOMA: Serikali kuboresha Afya ya mama na mtoto

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akijibu swali leo Bungeni mjini Dodoma.
    Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana akijibu maswali kutoka kwa wabunge jana mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoa maelezo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akitoa kauli ya Serikali kuhusu Mkakati wa Serikali wa Kutatua Changamoto za Soko la Sukari nchini, leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Susan Lyimo akichangia hoja ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) leo Bungeni mjini Dodoma.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Ester Bulaya akichangia hoja ya ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) jana Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Mkanyageni Mohamed Habibu Mnyaa akichangia hoja Bungeni mjini Dodoma leo wakati wa kuchangia hoja za Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri jana bungeni mjini Dodoma. (Picha zote na Hussein Makame-Maelezo, Dodoma)

Na Lorietha Laurence- Maelezo Dodoma
SERIKALI imeandaa  mikakati mbalimbali  ya  kuboresha afya ya wanawake wajawazito ili kupunguza vifo vitokanavyo na  uzazi.
Akijibu swali kwa Niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi, katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini  Dodoma, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana amesema moja ya mikakati hiyo ni  mpango mkakati ulioboreshwa wa kuendeleza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  uliozinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2014.

Alisema kuwa mpango huo unawashirikisha  wadau mbalimbali  ambao ni World Lung Foundation, Plan International, Care International, Jhpiego, UNFPA na GIZ  wanaochangia katika kupanua vituo vya  afya ,kujenga vyumba vya upasuaji na ununuzi wa vifaa na tiba.
“Mkakati  huu ni jitihada za serikali katika kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaboreshwa kwa kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi  na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano” alisema Dkt. Chana.
Alifafanua kuwa Rais Dkt Kikwete ameagiza  wakuu wa mikoa kusimamia masuala ya afya kwa  ngazi zote zinahusu afya ya mama na mtoto na kuhakikisha wanawasilisha taarifa za maendeleo ya utekelezaji kila baada ya miezi mitatu(3).  


Mpango mkakati huo umeanzishwa kutokana na bajeti finyu  ya  afya ya mama na mtoto ambayo imekuwa ikipungua kila mwaka wa  fedha  , hivyo serikali ikaona umuhimu wa kuangalia njia mbadala  ya kuweze kupata fedha ili kuongeza bajeti.

No comments:

Post a Comment