Mjadala mkali umeingia siku ya pili nchini Tanzania kufuatia Rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete kulihutubia taifa la nchi hiyo ambaye pamoja na mambo mengine alitangaza kumfuta kazi waziri mmoja kwa kuhusika na kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha kwenye account ya Escrow.
Upande wa upinzani umekosoa hotuba hiyo na kusema alipaswa kutangaza kuwafuta kazi mawaziri na watendaji wengine waliotajwa kwenye azimio la bunge lilipelekwa kwake hivi karibuni.Wakati haya yakiendelea wahisani waliositisha misaada kufuatia kashfa hiyo leo wamesema wamepokea kwa furaha hotuba hiyo na wametangaza kuanza kuipata Tanzania fedha asilimia 15 ya walizoahidi kwenye bajeti.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alitangaza kumfuta kazi waziri wa Ardhi Prof Anne Tibaijuka katika hotuba yake hapo jana ambaye ni mmoja ya mawaziri wanaodaiwa kuhusika na kashfa ya ufisadi ya kuhamisha isivyo halali fedha kwenya akaunti ya Tegeta Escrow.Hotuba hiyo Rais Kikwete tangu jana imezua mjadala mkali nchini Tanzania ambao wengi wamekuwa na maoni tofauti.
Chama Kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimekosoa hotuba hiyo na kusema kimesikitishwa na hatua alizozitangaza Rais Kikwete hapo jana.Hivi karibuni Bunge la Tanzania liliapitisha maazimio nane ambapo miongoni mwa maazimio hayo ilikuwa ni pamoja na serikali kuwachukulia hatua ZA kinidhamu pamoja na kuwafuta kazi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika katika sakata hilo.
Miongoni wa watendaji hao ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo Katibu Mkuu wa Wizara Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Profesa Anne Tibaijuka ,Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania Tanesco pamoja na maafisa wa na watendaji wengine waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo.
Hata hivyo katika hotuba hiyo Rais Kikwete mbali kumfuta kazi waziri huyo mmoja wa Ardhi hakusema kama hao waziri mwingine aliyebaki ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu wake watachukuliwa hatua za kinidhamu lini zaidi ya kusema anamweka kiporo waziri huyo huku akisubiri uchunguzi dhidi ya waziri huyo jambo linalopingwa na upande wa upinzani.
Wakati hayo yakiendelea nchi wahisani wa nchi zipatazo 12 ambazo zilisitisha misaada ya takribani dola milioni 500 kwenye bajeti ya Tanzania zimesema kupitia kwa Mwenyikiti wao ambaye balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila zimesema kwa njia ya barua pepe kwa BBC kuwa nchi hizo zimefurahishwa na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyokubali kutekeleza maazimio ya Bunge na kusema kuwa kuanzia kuanzia leo wamekubali dola bilioni 84 sawa na asilimia 15 ya mchango wao kwenye bajeti ya Tanzania.
Kwa upande mwingine upande wa chama kinachotawala CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wa vijana wa chama hicho Paul Makonda amesema wanaipongeza hotuba ya Rais Kikwete na hatua alizochukua.
Hotuba hiyo ya Rais Kikwete huenda itaendelea kuleta mjadala Tanzania kwa siku kadhaa kufuatia uzito wa kashfa hiyo ambayo imeitikisa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment