Serikali ya Sierra Leone imetangaza siku tatu za marufuku ya kutotoka nje kaskazini mwa taifa hilo, ili kuruhusu jitihada za kukabiliana na kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Msemaji wa serikali amesema kuwa maduka na masoko yatafungwa na hakuna magari ya abiria au pikipiki zitakubaliwa kwenye barabara za eneo hilo.
Sherehe za makanisa kuadhimisha sherehe za siku ya Krismasi pia zimepigwa marufuku.
Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa pakubwa na ugonjwa huo wa ebola.
No comments:
Post a Comment