TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

Maximo aaga Yanga arudi kwao Brazil

Marcio Maximo akimwonesha kitu Jerry Tegete wakati huo.
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo ameondoka jana kurudi nyumbani kwao Brazil na kuitakia klabu yake ya zamani kila la kheri.
Maximo na Mbrazil mwenzake, Leonardo Neiva wametupiwa virago na mabingwa hao wa zamani hivi karibuni kwa kile kinachoelezwa kufanya vibaya kwa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya vilabu ya shirikisho la soka Afrika hapo mwakani.‘Nawashukuru viongozi wa Yanga na mashabiki kwa muda tuliokaa pamoja”.” Yanga ni klabu kubwa yenye malengo”.
“Nilikuwa na malengo ya kuiongoza Yanga kitaalamu zaidi, lakini inaonekana fikra zangu hazikueleweka na kuungwa mkono”.
“Tayari kuna vilabu kadhaa vimeonesha nia ya kuniajiri lakini nitahitaji muda kidogo kufikiria”, alisema kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Maximo ameitumikia Yanga kwa miezi mitatu na kucheza mechi tisa. Katika hizo, amefungwa mechi mbili, moja hivi karibuni Yanga walipocheza na mahasimu wao Simba iliyochini ya kocha Mzambia Patrick Phiri na kufungwa 2-0 katika mechi isiyo ya ligi.

No comments:

Post a Comment