Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi
iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104,
waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini
India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. (Picha zote na
OMR)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9) Kutoka Zanzibar, mmoja
kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya
Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Zulekha
Said.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Yahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam,
mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Amina
Yahya.
Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam,
Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye
matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini
India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa
moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, waakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment