TANGAZO


Wednesday, December 24, 2014

IS:Yadungua ndege ya jeshi la muungano

Ndege ya jeshi la muungano unaoongozwa na marekani.
Wapiganaji wa Islamic State nchini Syria wamedai kuidungua ndege ya kivita ya muungano wa jeshi unaoongozwa na Marekani.
Shirika linalochunguza maswala ya haki za kibinadamu lenye makao yake mjini London ambalo linaunga mkono upinzani nchini Syria limesema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na mji wa kazkazini wa Raqqa unaodhibitiwa na IS.
Shirika hilo linasema kuwa rubani, raia mwarabu aliyekuwa akiendesha ndege hiyo ametekwa.
Baadhi ya ripoti zinadai kuwa rubani huyo ni raia wa Jordan.Jordan ni miongoni mwa mataifa ya kiarabu ambayo yanashiriki katika mashambulzi dhidi ya Islamic State.

No comments:

Post a Comment