Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36.
Maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika.
Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye mji wa Isangi ambapo mashua hiyo ilikuwa ikielekea
Nyumba kadha za serikali zinaripotiwa kuchomwa.
No comments:
Post a Comment