Kaimu Ofisa Mdhamini, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba, Khadija Khamis Rajab, akizungumza na wanakaya masikini za Junguni na Ukunjwi, Jimbo la Gando wilaya ya Wete kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wiliya hiyo. (Picha zote na Abdi Suleiman, PEMBA)
Mkuu wa Wilaya ya Wete, Mhe. Amran Massoud Amran, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Gando, wilayani Wete, ikiwa ni mara ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein, kushika wadhifa wa Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na wanakaya masikini za Junguni na Ukunjwi, Jimbo la Gando, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Gando katika ziara yake kisiwani Pemba leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na walimu wa Shule ya Msingi Kizimbani, Wilaya ya Wete, iliyofadhiliwa na TASAF, Awamu ya Pili, katika ziara yake kisiwani Pemba. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)
No comments:
Post a Comment