Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Manispaa
ya Kinondoni, John Chikomo akilifunga duka linalouza bidhaa hizo leo,
lijulikanalo kwa jina la Ng’aringa’ri lililopo eneo la Sinza jijini Dar es Salaam, kwa sababu halikusajiliwa. Anayeandika
maandishi ni Mfamasia Lucy Mziray na aliyesimama kulia ni Kaimu Msajili, Mboni Bakari,
wote kutoka Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala, lililochini ya Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii. (Picha zote na Magreth Kinabo- MAELEZO)
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Manispaa
ya Kinondoni, John Chikomo akilifunga duka linalouza bidhaa hizo leo,
lijulikanalo kwa jina la Ng’aringa’ri lililopo eneo la Sinza jijini Dar es Salaam, kwa sababu halikusajiliwa. Anayeandika
maandishi ni Mfamasia Lucy Mziray na aliyesimama kulia ni Kaimu Msajili, Mboni Bakari,
wote kutoka Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala, lililochini ya Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Timu ya ukaguzi wa vituo na maduka ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ikipata maelezo kuhusu shughuli za tiba hizo kutoka kwa mmiliki kituo cha Sure Herbal Clinic and Therapies, Simon Rusigwa kilichopo katika maeneo ya Sinza jijini Dares Salaam.
Timu ya ukaguzi wa vituo na maduka ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ikigua dawa katika kituo cha Praise Sanitarium Clinic. Anayeangalia kopo la dawa ni Mfamasia kutoka Bazara la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Lucy Mziray, anayesoma kitabu cha maelezo ni Kaimu Msajili wa Bazara la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Mboni Bakari na kulia ni Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Manispaa ya Kinondoni, John Chikomo.
Mashine ambayo hairuhusiwi kutumika ilikuwa ikitumika na Mtoa huduma wa kituo cha Praise Sanitarium Clinic, Peter Andew kilichopo katika maeneo ya Sinza jijini Dares Salaam kabla ya kuchukuliwa na Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Manispaa ya Kinondoni, John Chikomo(ambaye hayupo pichani) baada ya kufanyika ukaguzi chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Manispaa ya Kinondoni, John Chikomo (kulia) akitoka nje na mashine ambayo hairuhusiwi kutumika katika kituo cha Praise Sanitarium Clinic kilichopo katika maeneo ya Sinza jijini Dares Salaam baada ya kufanyika ukaguzi chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kushoto ni Mfamasia kutoka Bazara la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Lucy Mziray.
No comments:
Post a Comment