Bw. Said Seleman Jaffo
Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
ALIYEKUWA
mweka hazina wa Bunge la SADC ambaye pia ni Mbunge kutoka Bunge la Tanzania
Mhe. Said Seleman Jaffo ameutaka uongozi mpya wa Bunge la nchi wanachama wa
jumuiya ya kusini mwa Africa (SADC PF) kuendeleza mazuri yote yaliyoanchwa na
uongozi unaomaliza muda wake ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi bora ya
fedha za Bunge hilo kwa wanachama kwa lengo la kuendeleza Bunge hilo.
Mhe.
Jafo aliyasema hayo hapa mjini Victoria Falls alipokuwa akisomo taarifa ya
mapato na matumizi ya Bunge hilo kabla ya kukabidhi madaraka yake kwa uongozi
mpya uliochaguliwa jumapili iliyopita tarehe 2 Novemba, 2014.
Mhe. Jafo amesema, katika kipindi kifupi cha uongozi wake
kama mweka hazina ndani ya Bunge hilo,
aliweza kuweka utaratibu madhubuti wa kuzibiti matumizi ya fedha kwa
kuanzisha mfumo maalum uliosaidia kuhakikisha kuwa kila matumizi ya fedha ndani
ya Bunge hilo yanakuwa ya wazi na yanadhibiti na kirahisi kutokana na
mawasiliano yaliyopo:
“
Mfumo huu umetusaidia sana kuleta uwajibikaji ndani ya Bunge hili na hasa
katika kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha yote ndani ya Bunge hayaidhinishwi na
Sekretariati peke yake bali, Rais wa Bunge hili, Mweka Hazina pamoja kamati
tendaji wanakuwa wanapata taarifa za matumizi ya fedha kupitia mtandao jambo
ambalo si rahisi kwa mtu mmoja kufuja pesa kirahisi kwa kwa kuwa kila kitu kipo
katika mtandao” alisema Mhe. Jafo.
Mhe.
Jafo amsema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya uanzishwaji wa mfumo huu
wa kisasa Bunge hilo limeweza kufanikiwa kuondoa mapungufu yote yaliyokuwa
yakijitokeza mara kwa mara kama vile upungufu wa fedha na kushindwa kufikia
malengo kutokana na ukosefu wa fedha.
“
Napenda kuwafahamisha kuwa hadi kufikia mwezi machi, 2014, taarifa ya mkaguzi
wa hesabu za Bunge hili zilikuwa zinaonyesha kuwa tunaupungufu wa fedha, lakini
hivi ninavyowaambia mwezi huu November, kasoro hizo hamna tena bali tuna fedha
zaidi ndani ya bajeti yetu ambazo ni zaidi ya Dola 824,000” aliongeza Mhe.
Jafo.
Akizungumza
nje ya ukumbi baada ya kuwasilisha ripoti hiyo ya fedha na baadae kumkabidhi
mweka hazina mpya mikoba ambaye ni Mhe. Gary Nkombo kutoka Zambia, Mhe. Jafo
amesema uanzishwaji wa mfumo huo wa udhibiti wa matumizi ya fedha, sio tu
umelisaida Bunge hilo bali umeipa sana heshima nchi yetu kwa kuwa utaratibu huu
ni mpya na umeonyesha mafanikio ndani ya kipindi kifupi sana.
Anasema
zamani, viongozi walikuwa hawana mawasiliano ya moja kwa moja ya nini kinafanyika
na fedha za Bunge lakini baada ya kuazishwa kwa mfumo huu kila kitu kipo wazi
na hakuna anaweza kufishwa taarifa yoyote inayohusu fedha kama vile manunuzi,
mikataba, mikopo, misaada na michango mbalimbali kutoka kwa wahisani nk.
Mhe.
Jafo alichukua nafasi ya uweka Hazina mwezi june mwaka huu baada ya aliyekuwepo
katika nafasi hiyo Mhe. Dkt. Titus Kamani kuchaguliwa katika baraza la
Mawaziri.
No comments:
Post a Comment