TANGAZO


Monday, November 3, 2014

Homa ya Lassa haijatiliwa maanani

Ebola imekua tishio Afrika Magharibi kiasi cha kusahau homa ya Lassa
Ugonjwa wa homa ya Lassa Afrika Magharibi unaelezwa kusahaulika kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na Wahudumu wa afya wamesema huenda wakakosa rasilimali kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utakithiri.
Awali dalili za homa hii zilionekana kama za ugonjwa wa ebola.kuvuja damu, kutapika na joto kali la mwili.lakini kwa kuwa ebola ni ugonjwa mpya, homa ya Lassa nayo bado ipo, ambayo inaelezwa kuwa kila mwaka watu 300,000 mpaka 500,000 huathiriwa na homa hii na watu mpaka 20,000 hupoteza maisha.
Kila nchi iliyoathiriwa na ebola pia ina ugonjwa wa homa ya Lassa, ijumaa juma lililopita Dr.Geraldine O'Hara kutoka Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF ameiambia BBC kuwa mmoja wa wafanyakazi wenzake alipoteza maisha ingawa walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake.
Inaelezwa kuwa Nigeria huenda ikakumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Lassa, wakati huu ikiwa ni majuma kadhaa baada ya kufanikiwa kukabili ugonjwa wa ebola.
Kuna tofauti moja kubwa kati ya ebola na homa ya Lassa.Lassa husababishwa na Panya ambao hubeba vijidudu kwenye maeneo ya makazi ya watu na kwenye hifadhi za vyakula hasa kipindi cha Kiangazi.
Profesa Robert Garry kutoka Chuo cha Tulane amefanya utafiti kuhusu ugonjwa huu kwa amesema Kumekua na ripoti kadhaa za watu kuugua homa ya Lassa nchini Sierra Leone.
Lassa huambukiza lakini si kila anayeambukizwa huwa katika hali mbaya, ugonjwa huu hausambai kwa kasi kama ebola.

No comments:

Post a Comment