TANGAZO


Sunday, November 30, 2014

Wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET) Kampasi ya Kijitonyama waelimishwa kushiriki shindano la App star

Wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET), Kampasi ya Kijitonyama wakimsikiliza kwa makini mmiliki wa mtandao wa Popote Media, Gillbart Mlaseko (kushoto), alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusu shindano la AppStar linaloendeshwa na Vodacom Tanzania linalohusu ubunifu wa program za simu za mkononi. Washindi watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na Barcelona kushiriki katika shindano hilo ngazi ya Kimataifa. Wapili kushoto ni Meneja Uhusoiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni. 

Mmoja wa wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COET), Kampasi ya Kijitonyama akimuuliza swali mshindi wa shindano la App Star mwaka 2012, Ernest Mwalusanya kuhusu na shindano la AppStar linaloendeshwa na Vodacom Tanzania linalowalenga wabunifu wa program za simu za mkononi ambapo washindi  watajishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na Barcelona kushiriki katika shindano hilo katika ngazi ya Kimataifa.
Mshindi wa shindano la AppStar mwaka 2012 Ernest Mwalusanya, akiwafafanulia jambo baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi ya Kompyuta kuhusu jinsi ya kushiriki katika shindano la AppStar, linaloendeshwa na Vodacom Tanzania. Shindandano hilo ni mahususi kwa wataalamu wabunifu wa kutengeneza mobile applications. Washindi watajishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo pesa taslim na safari za kwenda nchini India na Barcelona kushiriki katika shindano la ngazi ya Kimataifa. (Picha zote na mpigapicha wetu)

Rais Kikwete alivyopokelewa kwa shangwe Ikulu

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwapungia wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam jana, akitokea nchini Marekani ambako alifanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwapungia wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam jana, akitokea nchini Marekani ambako alifanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili Ikulu jijini jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili Ikulu jijini jana.
Mjukuu wa Rais Kikwete, Aziza Ridhiwani Kikwete akimpokea kwa shangwe na kadi Babu yake na kisha kupiga naye soga mara
baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal aiwakilisha Tanzania Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu jijini Nairobi, Kenya


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. (Picha zote na OMR)

Na Ofisi ya Makamu wa Rais
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya.
 


Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.

Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.

Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. 


Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  

Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.

Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. 
Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi yapokea msaada wa Pikipiki 10 kutoka Dalbit Petrolium


Kamishina wa oporesheni na mafunzo  wa jeshi la polisi, Paulo Chagonja akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa pikipiki 10 aina ya boxes kutoka kwa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium ya nchini  kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani. Katikati ni  Mwenyekiti wa kampuni  Hum Dalbit Petrolium Humprey Kariuki na Kushoto ni Mkurugenzi wa maswala ya Uhusiano wa Kampuni hiyo Magaret Mbaka.



Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiangalia  pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.



Kamishina wa oporesheni na mafunzo  wa jeshi la polisi Paulo Chagonja akijaribu kuendesha moja ya pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kwa kupambana na waalifu wa makosa mbalimbali. Kulia aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Humprey Kariuki.


Kamishina   wa oporesheni na mafunzo  wa jeshi la polisi Paulo Chagonja akijaribu kuendesha moja ya pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kwa kupambana na waalifu wa makosa mbalimbali. Kulia aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Humprey Kariuki.




Mwenyekiti wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini Hamphrey Kariuki akipongezana na Kamishina   wa oporesheni na mafunzo  wa jeshi la polisi nchini Paulo Chagonja  baada ya hafla ya kukabidhiana msaada wa  pikipiki 10 aina ya boxes  kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuisha. Wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa Usalama barabarani Mohammed Mpinga hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.



Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiangalia msaasa wa pikipiki 10 aina ya boxes zilizotolewa na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani ilikupambana na  kubaini makosa mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mpigapicha wetu)