TANGAZO


Sunday, October 5, 2014

Wadau wa Kilimo cha Pamba Wilaya ya Bunda mkoani Mara wakutana kujadili changamoto za zao hilo

Bw. Japhet Kwangula akieleza katika Mkutano wa wakulima wa pamba uliofanyika hivi karibuni wilayani Bunda juu ya umuhimu wa kupata pembejeo kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa. Katika mkutano huo, wakulima waliweza kupata fursa ya kujadili ya mafanikio na changamoto zilizopo kwenye sekta ya pamba sambamba na kujadiliana namna ya kupata njia sahihi ya kuwawezesha kufanya vizuri na hivyo kufikia malengo kwa msimu ujao.
Mmoja ya wakulima wa pamba akichangia katika majadiliano juu ya faida ya kilimo cha mkataba kwenye mkutano wa wakulima wa pamba uliokuwa ukichambua juu ya mafanikio, changamoto na njia sahihi za kuweza kufanya sekta hiyo kuendeshwa kwa mafanikio zaidi kwa msimu ujao. Mkutano huo ulifanyika wilayani Bunda hivi karibuni.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Bw. Dominicas Lusasi akiongea na wakulima wa wilaya hiyo kwenye majadiliano yaliyolenga kuwapa wakulima wa Bunda  motisha kwa kuwa na pamba yenye ubora wa hali ya juu. Mkutano huo wa wakulima wa pamba ulifanyika hivi karibuni wilayani Bunda. Mkutano huo uliwapa fursa wakulima ya  kujadili ya mafanikio na changamoto katika sekta ya pamba sambamba na kujadiliana njia bora ya kuwezesha kufanya vizuri na kufikia malengo kwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment